KK Fosu

Mwanamuziki wa Ghana

Kaakyire Kwame Fosu, (alizaliwa 14 Februari, 1981) ni mwanamuziki wa hiplife wa nchini Ghana anayejulikana kwa jina la kisanii la KK Fosu. Anajulikana zaidi kwa nyimbo kama "Suudwe", "Anadwo Yede" na nyingine nyingi.[1]

Maisha na kazi hariri

KK Fosu alianza muziki akiwa na umri mdogo akiwa katika kwaya ya shule alipokua Sekondari. [2] Alijiunga na kundi la bendi moja kwa moja lililoitwa "Soundz Unlimited" ambapo alicheza kwa miaka miwili. Baadaye alisainiwa na lebo ya DKB.

KK Fosu ametoa albamu tano ambazo ni "Sudwe", "Anadwo Yede", "6'oclock", Akonoba na "Toffee". Amefanya kazi na wanamuziki kama Obrafour,Obour, Reggie Rockstone na wengine kadhaa. [3]

Marejeo hariri

  1. "Deplorable state of Mangoase, Adawso and Tinkong roads affecting transportation of farm produce - Residents lament - MyJoyOnline.com". www.myjoyonline.com (kwa en-US). 2021-08-13. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  2. "K.K Fosu: A combination of the old and new". ghananewsagency.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-03. Iliwekwa mnamo 2020-02-03. 
  3. "KK Fosu". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2016-07-19. Iliwekwa mnamo 2020-02-03.