Karroo

eneo kubwa la nusu jangwa nchini Afrika Kusini

Karoo (pia Karroo tamka Karu) ni eneo la nusu jangwa katika nyanda za juu za Afrika Kusini. Inaenea kaskazini mwa mtelemko mkubwa ambako nyanda za juu zinaanza na kusini mwa Namibia. Hapa Karoo Ndogo, Karoo Kubwa na Karoo ya Juu zinatofautishwa pamoja na Karoo ya Sukulenti na Karoo ya Wanama. Ikiwa na eneo la kilomita 500,000 za mraba, Karoo inajumuisha karibu theluthi moja ya eneo la Afrika Kusini.

Hifadhi ya Kitaifa ya Karoo
Kanda mbili za Karoo kulingana na WWF

Hakuna ufafanuzi kamili wa Karoo kwa hiyo hakuna mipaka maalumu. Mfafanuzi hutegemea uso wa nchi, jiolojia, tabianchi na hasa kiasi kidogo cha mvua pamoja kutokea kwa baridi na joto kali.[1][2] Miaka milioni iliyopita Karoo ilikuwa na mfumo wa ikolojia wa pekee inayoonekana hado leo katika visukuku vingi.[3]

Hadi leo ni mazingira ya joto kali pamoja na jalidi. Mvua inanyesha kwa wastani milimita 50 hadi 250 kwa mwaka, lakini kwene milima kadhaa hufikia milimita 250 hadi 500.[4] Maji hupatikana chini ya ardhi yanayopatikana kwa njia ya visima vilivyochimbwa.[4][5]

Marejeo hariri

  1. Potgieter, D.J. & du Plessis, T.C. (1972) Standard Encyclopaedia of Southern Africa. Vol. 6. pp. 306–307. Nasou, Cape Town.
  2. Reader’s Digest Illustrated Guide to Southern Africa. (5th Ed. 1993). pp. 78–89. Reader’s Digest Association of South Africa Pty. Ltd., Cape Town.
  3. Sahney, S.; Benton, M.J. (2008). "Recovery from the most profound mass extinction of all time". Proceedings of the Royal Society B: Biological Sciences 275 (1636): 759–65. PMC 2596898. PMID 18198148. doi:10.1098/rspb.2007.1370. 
  4. 4.0 4.1 Potgieter, D.J. & du Plessis, T.C. (1972) Standard Encyclopaedia of Southern Africa. Vol. 6. pp. 306–307. Nasou, Cape Town.
  5. Reader’s Digest Illustrated Guide to Southern Africa. (5th Ed. 1993). pp. 78–89. Reader’s Digest Association of South Africa Pty. Ltd., Cape Town.