Kaunti ya Uasin Gishu

Kaunti ya Uasin Gishu ni mojawapo za kaunti za Kenya zilizobuniwa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupitishwa mwaka 2010. Uasin Gishu ni kaunti nambari 27 kulingana na orodha uliobuniwa kurahisisha utambulizi.

Ramani ikionesha eneo la Kaunti ya Uasin Gishu, Kenya.

Wakati wa sensa uliofanyika mwaka 2019 ,idadi ya wakaazi ilikuwa 1,163,186 katika eneo la km2 3,392.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 343 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Eldoret.

Utawala hariri

Kaunti ya Uasin Gishu imegawiwa katika maeneo bunge yafuatayo:

Eeneo bunge Kata
Ainabkoi Kapsoya, Kaptagat, Ainabkoi/Olare
Kapseret Simat/Kapseret, Kipkenyo, Langas, Megun, Ngeria
Kesses Cheptiret/Kipchamo, Racecourse, Tulwet/Chuiyat, Tarakwa
Moiben Karuna/Meibeki, Kimumu, Moiben, Sergoit, Tembelio
Soy Kapkures, Kipsomba, Kuinet/Kapsuswa, Moi's Bridge, Segero/Barsombe, Soy, Ziwa
Turbo Huruma, Kamagut, Kapsaos, Kiplombe, Ngenyilel, Tapsagoi

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [2] hariri

  • Ainabkoi 138,184
  • Kapseret 198,499
  • Kesses 148,798
  • Moiben 181,338
  • Soy 229,094
  • Turbo 267,273

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.