Kerrea Gilbert

Wachezaji mpira wa Uingereza

Kerrea Kuche Gilbert (alizaliwa Hammersmith, London, 28 Februari 1987) alikuwa mchezaji wa kandanda wa Uingereza NA wa klabu ya Arsenal FC kama mlinzi.

Kerrea Gilbert
Maelezo binafsi
Jina kamili Kerrea Kuche Gilbert
Tarehe ya kuzaliwa 28 Februari 1987
Mahala pa kuzaliwa    Hammersmith,London, Uingereza
Urefu 1.75m
Nafasi anayochezea Difenda
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 42
Klabu za vijana
2003–2005 Arsenal FC
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2005-
2006-2007
2007-2008
2008-2009
Arsenal
Cardiff
Southend United
LeicesterCity
Timu ya taifa
Uingereza

* Magoli alioshinda

Kazi hariri

Arsenal hariri

Gilbert alikuwa akicheza katika timu za vijana na timu hifadhi mpaka msimu wa 2005-06. Hata hivyo, baada ya majeruhi kwa wachezaji kadhaa katika timu ya Arsena ,Gilbert aliorodheshwa kama mchezaji mbadala wa difenda wengine. Alichezea timu ya kwanza kwa mara ya kwanza dhidi ya Reading katika Shindano la Kombe la League mnamo 29 Novemba 2005.Mnamo tarehe 7 Desemba alicheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA dhidi ya Ajax Amsterdam akiwa mchezaji mbadala kwa Lauren aliyekuwa ameumia.

Shida ya majeruhi katika timu ya Arsenal iliendelea ,ikampa nafasi ya kuanza mechi dhidi ya Cardiff City katika Shindano la Kombe la FA mnamo 7 Januari 2006.Alisifiwa kwa mbio zake za kasi na akacheza katika mechi sita baada ya mechi hiyo. Alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza mnamo 21 Januari 2006 katika mechi dhidi ya Everton, walishindwa 1-0.Alicheza pia katika mikondo yote miwili ya nusu fainali ya Shindano la Kombe la League dhidi ya Wigan Athletic,alisaidia katika kufunga kwa bao la Thierry Henry.Arsenal walishindwa kwa shindano hilo.

Hata hivyo, Gilbert mwenyewe alipata majeraha katika mechi ya Arsenal na West Ham mnamo 1 Februari 2006,walishindwa 3-2.Alikatazwa kucheza kwa miezi miwili,hivyo basi ikamnyang'anya nafasi ya timu. Tangu Aprili 2006, amechezea timu ya Arsenal mara 9.

Cardiff City hariri

Tarehe 21 Julai 2006, Gilbert alihamia timu ya Cardiff City katika mpango wa mkopo katika msimu wa 2006-07. Gilbert alianza msimu katika klabu hiyo kama difenda wa upande wa kulia na akacheza mara kwa mara katika timu hiyo hadi Desemba. Hata hivyo,alipata majeraha madogo yaliyomfanya asicheze mechi kadhaa. Nafasi yake ilichukuliwa na Chris Gunter na hakuweza kumtoa Chris hapo na hakucheza sana katika mechi zilizobaki katika msimu huo. Gilbert akacheza mechi 26 katika timu hiyo ya Cardiff.

Southend United hariri

Yeye alijiunga na Southend United kwenye mpango wa mkopo wa miezi sita mnamo tarehe 30 Julai 2007. [5] Alicheza mechi sita katika timu hiyo ya Southend kabla ya kutopendwa na meneja Steve Tilson na kutohusishwa katika timu. Yeye alirudi timu ya Arsenal mnamo tarehe 3 Januari 2008. [7]

Kurudi Arsenal hariri

Baada ya kurudi timu ya Arsenal, Gilbert alipewa jezi ya # 46 na akaorodheshwa kama mchezaji mbadala katika mechi ya ligi dhidi ya Blackburn mnamo 11 Februari 2008,hakucheza mechi hiyo.

Leicester City hariri

Tarehe 10 Julai 2008, Gilbert alijiunga na Leicester City katika mpango wa mkopo wa msimu mzima wa 2008-2009. Yeye alifunga bao lake la kwanza ya ligi yake katika mechi dhidi ya Stockport County iliyoisha 1-1.

Kurudi Arsenal hariri

Katika msimu wa 2009-10, Gilbert alirejea Arsenal. Yeye alicheza katika mechi ya Arsenal dhidi ya West Bromwich Albion katika Shindano la Kombe la League,akicheza dakika zote 90 huku wakishinda 1-0. Kerrea ,pia, alicheza katika Shindano la Kombe la League waliposhinda Liverpool 2-1. Alishiriki katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa baada ya miaka minne,dhidi ya Olympiakos.Timu iliyocheza siku hiyo ilikuwa timu kijana kabisa kucheza katika shindano hilo ikiwa na umri wa miaka 21,hii ilivunja rekodi ya hapo awali iliyoshikiliwa na Ajax.

Takwimu ya Wasifu hariri

(sahihi tangu 9 Desemba 2009)
Klabu Msimu Ligi Mashindano ya kombe yote Uropa(Ligi ya Mabingwa ya UEFA) Total
Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao
Arsenal 2005–06 2 0 6 0 1 0 9 0
2006–07 Msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo
2007–08 Msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo
2008–09 Msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo
2009–10 0 0 2 0 1 0 3 0
Cardiff City 2006–07 24 0 2 0 - 26 0
Southend United 2007–08 5 0 1 0 - 6 0
Leicester City 2008–09 34 1 5 0 - 39 1
Jumla 2005– 65 1 16 0 2 0 83 1

*KUMBUKA timu katika Kiitaliki inaonyesha msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo in

Tuzo hariri

Leicester City
  • Ligi ya Kwanza ya Uingereza : 2008–09

Marejeo hariri

  1. BBC Sport. 2006-07-21. "Cardiff sign Glombard and Gilbert"
  2. BBC Sport. 2007-07-30. "Arsenal's Gilbert joins Southend".
  3. Yahoo! Sports. 2008-01-03. "Shrimpers bid Gilbert farewell".
  4. BBC Sport. 2008-07-10. "Leicester sign Arsenal's Gilbert".
  5. "Leicester 1-1 Stockport". BBC. 3 Machi 2009. "Leicester 1-1 Stockport".

Viungo vya nje hariri