Ket (kwa Kirusi: Кеть) ni mto ulioko Urusi; una urefu wa kilometa 1,621.

Tomsk Oblast, Beseni la Ob na Ket.

Ket ni tawimto la mto Ob unaopeleka maji yake hadi Bahari ya Aktiki. Mkondo wake mdomoni ni mita za ujazo 469 kwa sekunde.

Ket ina chanzo chake katika Krasnoyarsk Krai ikiendela katika Tomsk Oblast. Ni kati ya mito ya Urusi yenye mwendo kutoka mashariki kuelekea magharibi; hivyo ilikuwa njia muhimu ya usafiri katika historia ya Siberia ambayo ni eneo kubwa la Urusi lenye barabara chache.

Kuanzia Novemba hadi Aprili au Mei maji yake huganda kuwa barafu.

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ket kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.