Khadja Nin (amezaliwa tar. 27 Juni 1959) ni mpiga muziki na mwimbaji mashuhuri barani Afrika na ulimwenguni kutoka nchi ya Burundi mwenye uraia wa Ubelgiji.

Khadja Nin
Khadja Nin katika Tamasha la Filamu la Cannes 2018
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaKhadija Nin
ChimbukoBurundi

Alizaliwa Burundi mdogo katika familia yenye kujengwa na watu wa nane. Baba yake alikua mwanasiasa. Khadja Nin alisomea kuimba katika umri wake mdogo kama vile ndugu zake wakike na wakiume karibia wote walikua waimbaji. Khadja Nin alikua na sauti ya kipekee nzuri, katika umri wa myaka mi 7 wakati huo alitokea kua muimbaji wa nyimbo za kwaya Kanisa la Katedrali na sauti yake ilikua sauti ya nyororo ambayo ilikua ikiwavutia hadi wafata ibada Kanisani. Mwaka 1975 Khadja Nin aliiacha Burundi kuelekea Zaire kwa sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na alifaanikisha kuolewa mwaka 1978. Katika mwaka 1980 alihamia Ubelgiji pamoja na mtoto wake wa myaka miwili. Katika mwaka 1985 alikutana na muimbaji Nicolas Fiszman ambaye alimsaidia Khadja Nin kuweza kufunga mapatano na shirika lakutoa miziki la BMG linalopatikana Gütersloh, Ujerumani. Albamu yake ya pili ya mwaka 1994 ilitolewa ikiwa na anuani ya jina la (Ya pili) ilipata umashuhuri na ndio alikuja kutokea kua maarufu kwa albumu hiyo, na hivyo, mwaka 1996 alitoa albumu kali mashuhuri ambayo ilipata wapenzi wengi zaidi na anuani ya albamu hiyo ni Sambolera, ambayo aliimba kwa lugha tatu Kiswahili, Kirundi na Kifaransa. Khadja Nin alifaanikisha kwakutumia kwa upana namna yakuimba baina ya mwendo wa pigo la muziki wakiafrika na muundo wa kisasa wa muziki wa pop (chomoka) ili kuweza kujitengenezea soko la kibiasha kwa muziki na jambo hilo alifaanikisha. Miongoni ya nyimbo zake zilizopendwa na watu ni (Sina Mali, Sina Deni), ambao ulifasiriwa katika funikio la chapisho ya albamu ya muimbaji mashuhuri Stevie Wonder muziki wake wa bure.

Diskografia hariri

Hii ni baadhi ya sehemu ya albamu za Khadija Nin;

Marejeo ya nje hariri

  Makala hii kuhusu muziki wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khadja Nin kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.