Kirangi (kwa kilugha Kilangi) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Warangi. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kirangi imehesabiwa kuwa watu 410,0000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kirangi iko katika kundi la F30.

Mfumo wa Sauti (Fonolojia) hariri

Lugha ya Kirangi ina irabu 7 na konsonanti 22. Pia tofauti kati ya irabu fupi na irabu ndefu huleta tofauti za maana. Tena, kuna toni (au mawimbi ya sauti) zinazotofautisha maana ya nomino fulani, na nyakati za vitenzi.

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri

  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

  • Dempwolff, Otto. 1915/16. Beiträge zur Kenntnis der Sprachen in Deutsch-Ostafrika. Teil 8: Irangi (Langi). Zeitschrift für Kolonialsprachen, 6, uk.102-123.
  • Seidel, August. 1898. Grammatik der Sprache von Irangi. Katika: Die mittleren Hochländer des nördlischen Deutsch-Ostafrika, uk.387-435. Kuhaririwa na C. Waldemar Werther. Berlin: Verlag von Hermann Paetel.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kirangi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.