Kiruna (kisami ya kaskazini: Giron; Kifini: Kiiruna) ni mji na manispaa ya kaskazini kabisa nchini Uswidi. Kuna wakazi 18,154 (mwaka 2005).

Kiruna

Kiruna ni mji ulioanzishwa 1899 kama kituo cha migodi ya kuchimba chuma. Mwaka uleule njia ya reli ilikamilishwa hadi mahali pa mji mpya iliyokuwa lazima kwa kubeba madini ya chuma. Mji uko katikati ya milima miwili yenye asilimia kubwa ya madini ya chuma.

Uchimbaji chuma umeshamaliza akiba juu ya uso wa ardhi na kuendelea chini ya ardhi. Kwa sababu hiyo mji uliojengwa juu ya madini utahamishwa umbali wa kilomita 5 ili kuwezesha kuchimbwa chini ya mji wa sasa.

Jiografia hariri

Eneo lake ni 15.95 km².

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Uswidi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kiruna kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.