Kiserbokroatia (iliyoitwa pia Kikroatoserbia, halafu pia "Kiserbia au Kikroatia" na "Kikroatia au Kiserbia" - srpskohrvatski au српскохрватски au hrvatskosrpski au hrvatski ili srpski au srpski ili hrvatski) ilikuwa lugha rasmi ya Yugoslavia pamoja na Kislovenia na Kimasedonia.

Wakati wa Ufalme na baadaye Jamhuri ya Yugoslavia Kiserbia na Kikroatia zilitazamwa kama lahaja za lugha moja iliyoendelea kwa karne nyingi katika eneo lililogawiwa kisiasa. Taifa jipya ya Yugoslavia lilitaka kuunganisha lahaja za karibu za Wakroatia, Waserbia na Wabosnia. Huo ulikuwa mpango wa kuunda lugha sanifu ya kisasa na kujenga umoja wa kitaifa.

Kufuatana na tamaduni mbalimbali katika Yugoslavia lugha hiyo iliandikwa kwa alfabeti ya Kikirili upanda wa Mashariki katika eneo la Serbia na kwa alfabeti ya Kilatini upande wa Magharibi katika eneo la Kroatia.

Baada ya kusambaratika kwa Yugoslavia tangu mwaka 1991 maeneo yake yaliendelea kama nchi huru za pekee. Kila nchi kati ya Serbia, Kroatia, Bosnia-Herzegovina na hatimaye Montenegro ilianza kudai ya kwamba lugha ya watu wake ni lugha ya pekee. Neno na wazo la "Kiserbokroatia" lilifutwa kati ya wasemaji wa lugha baada ya kipindi cha uadui na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo wataalamu wengi wanaiona bado kuwa lugha moja.

Mifano ya tofauti kati ya lahaja hizo hariri

Français Kikroatia Kibosnia Kiserbia
Comme les gaz d'échappement et la pollution atmosphérique dans la Jérusalem, il serait nécessaire de prendre des mesures pour assurer la sécurité! Glede ispušnih plinova i zagađivanja zraka u Jeruzalemu, bilo bi potrebito poduzeti mjere sigurnosti! U pogledu izduvnih gasova i zagađivanja vazduha u Jerusalimu, bilo bi potrebno preduzeti mjere bezbjednosti! У погледу издувних гасова и загађивања ваздуха у Јерусалиму, било би потребно предузети мере безбедности!

Viungo vya nje hariri