Kolo ni kata ya Wilaya ya Kondoa Mjini katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41704[1].

Kata ya Kolo
Nchi Tanzania
Mkoa Dodoma
Wilaya Kondoa Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 5,649

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,649 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5243 [3] waishio humo.

Kolo iko kwenye barabara kuu kati ya Babati na Kondoa.

Baadhi ya vijiji vya kata ya Kolo vyenye shule ya msingi ni Kolo yenyewe, Bolisa, Gubali, Hachwi na Itiso. Asilimia kubwa za wakazi wa kata ya Kolo ni Warangi, ingawa zamani ilikuwa eneo la Waalagwa.

Shule ya msingi ya Kolo ilifunguliwa mwaka wa 1917 ikiwa ni shule ya kwanza katika wilaya ya Kondoa. Ilifunguliwa chini ya utawala wa Sultani Salimu Kimolo ambaye ikulu yake bado ipo katika kijiji cha Kolo.

Pia, kata ya Kolo ni maarufu kama mahali pa kufikia kwa michoro ya Kondoa kwa sababu hapa barabara kuu inafika karibu na sehemu ya michoro hii.

Michoro ya kale karibu na Kolo

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08. 
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. "Sensa ya 2012, Dodoma - Kondoa DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-18. 
  Kata za Wilaya ya Kondoa Mjini - Mkoa wa Dodoma - Tanzania  

Bolisa | Chemchem | Kilimani | Kingale | Kolo | Kondoa Mjini | Serya | Suruke


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kolo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.