Kolojojo

Ndege wadogo wa jenasi Macrosphenus, familia Macrosphenidae
Kolojojo
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Macrosphenidae (Ndege walio na mnasaba na kolojojo)
Jenasi: Macrosphenus
Cassin, 1859
Ngazi za chini

Spishi 5:

Kolojojo ni ndege wadogo wa jenasi Macrosphenus ambao zamani waliainishwa katika Sylviidae, familia ya kucha. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba labda ndege hawa ni kundi lao lenyewe pamoja na vikucha na spishi nyingine za kucha wa Afrika. Kwa sasa hakuna uhakika kama ndege hawa wote waunda familia yao au wamo katika familia mbalimbali. Kufuatana na uchanganuzi wa juzi wa DNA inawezekana kama spishi moja, Macrosphenus kretschmeri, si kolojojo lakini aina ya korogoto au nyembelele. Kolojojo wanafanana na shoro, kuchanyika na kuchamsitu ambao zamani waliainishwa pia katika familia Sylviidae, lakini kolojojo ni wadogo zaidi na wana domo refu na mkia mfupi lakini si mfupi kama ule wa vikucha. Rangi yao kuu ni zaituni, njano tumboni na njano, machungwa au nyekundu mbavuni. Hula wadudu ambao huwatafuta kwa mashina na matawi ya miti na mitambaa. Mwenendo wao wa kuzaa na kujenga tago haujulikani.

Spishi za Afrika hariri