Koose (pia inajulikana kama Keki ya Maharagwe) ni mkate wa kunde wenye macho meusi ambao huliwa sana Afrika Magharibi kama vitafunio.

Picha ya Koose
Picha ya Koose

Ilianzishwa kwa Afrika Magharibi na watu wa Hausa wa Kaskazini mwa Nigeria na maeneo mengine ya Afrika Magharibi kama vile eneo la kaskazini la Ghana, Sierra Leone na KamerunI. Koose pia inaweza kupatikana katika nchi za Caribbean kama vile Kuba na katika nchi za Amerika Kusini kama vile Brazili. Inajulikana nchini Ghana kama "koose" au "koosay", nchini Nigeria kama "akara", nchini Brazili kama "acaraje" na nchini Kuba kama "bollitos de carita". Kwa Dagbamba wa Ghana inajulikana kama "Kooshe", Waewe wanaiita "agawu" na kwa baadhi ya jamii ya Zongo kama "koose tankuwa".

Marejeo hariri