Krodegango (alizaliwa Hesbaye, leo nchini Ubelgiji; alifariki Metz, leo nchini Ufaransa, 6 Machi 766) alikuwa askofu wa mji huo tangu mwaka 742 au 748 akibaki chansela wa mfalme Karolo Nyundo, ndugu yake.

Mt. Krodegango katika kioo cha rangi.

Alidai waklero wanajimbo waishi kama monasterini akaandika pia kanuni maarufu kwa jumuia zao za kikanoni iliyoandaa urekebisho wa Kanisa la Ulaya magharibi utakaofanywa na kaisari Karolo Mkuu[1][2][3]. Pia alistawisha uimbaji katika liturujia.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.