Lameki ni jina la watu wawili wa Agano la Kale katika Biblia.

Lameki akimuua Kaini (kushoto) kadiri ya hadithi fulani iliyochongwa na Wiligelmo huko Modena (Italia).

Kitabu cha Mwanzo katika 4:18-24 kinamtaja mmojawao kama mwana wa Metusala katika kizazi cha tano baada ya Kaini. Ndiye wa kwanza kuoa mitara akiwa na wake wawili, Ada e Zila, waliomzalia watoto wanne: Jabal, Jubal, Tubalkain na Naama (huyo wa mwisho akiwa mwanamke). Kila mmojawao anawakilisha fani fulani: uchungaji, muziki, uhunzi na labda umalaya.

Lameki anakumbukwa pia kama mtu wa kisasi kikali.

Kitabu hichohicho kinamtaja Lameki mwingine katika 5:28, mwana wa Metusala katika kizazi cha saba baada ya Seti. Ndiye baba wa Nuhu.