Leopold II wa Ubelgiji

Leopold II alikuwa mfalme wa Ubelgiji tangu 10 Desemba 1865 hadi 17 Desemba 1909. Alimfuata babake Leopold I aliyekuwa mfalme wa kwanza wa nchi baada ya kuanzishwa kwa taifa hili.

Leopold II wa Ubelgiji

Mfalme wa nchi ndogo na mfanyabiashara hariri

Kisiasa hakuwa na umuhimu sana kwa sababu nchi yake ilikuwa ndogo tena nafasi ya mfalme katika Ubelgiji haikuwa na mamlaka kubwa. Lakini Leopold II alifaulu kama mwanabiashara aliyetafuta kila njia ya kuongeza mali yake. Kwa njia hii alianza kujihusisha na habari za Afrika na hasa Kongo.

Kuunda ufalme mpya katika Kongo hariri

Leopold ailifaulu kujipatia utawala juu ya maeneo makubwa ya beseni ya Kongo kama mali ya kampuni ya binafsi ambamo yeye mwenyewe alikuwa na hisa nyingi. Leopold alishirikiana na mpelelezi Henry Morton Stanley aliyeweka misingi kwa yote yaliyotokea baadaye. Kwa njia hii alielekea kufanya Kongo kuwa mali yake ya binafsi. Baada ya kutawala sehemu za Kongo alitafuta utambulizi wa utawala wake kutoka nchi mbalimbali. 1884 Marekani ilitambua "Dola huru ya Kongo". Sasa athira yake ilikuwa kubwa kiasi ya kusababisha mashindano kati ya mataifa mengine ya Ulaya juu ya athira katika Afrika. Mkutano wa Berlin wa 1885 ilikubali "Dola huru la Kongo" kama nchi ya kujitegemea iliyokuwa mkononi mwa shirika la Leopold.

Leopold mwenyewe hakukanyaga ardhi ya Kongo. Nia yake ilikuwa utajiri pekee. Alifaulu kijitajirisha lakini bei kali ililipiwa na watu wa Kongo.

Njaa ya mpira hariri

Badala ya kulinda wenyeji dhidi ya biashara ya watumwa jinsi alivyotangaza kote duniani alikodi malighafi za Kongo kwa watu na makampuni waliompa pesa. Makampuni haya yalipewa mamlaka ya kulazimisha wenyeji kuwafanyia kazi ya lazima kama kubeba mizigo na kukusanya mpira msituni. Leopold alitajirika kwa sababu teknolojia mpya ya matairi ilihitaji kiasi kikubwa cha mpira iliyopatikana pekee katika misitu ya nchi za tropiki kama Kongo. Baadaye mashamba ya mipira ilianzishwa lakini wakati ule viwanda vilitumia mpira asilia.

Unyama wa Leopold hariri

Wakala wa Leopold walidai kila kijiji kilete kiasi fulani cha mpira. Kama hakikuletwa walitoa adhabu kali kwa kusudi ya kutisha wengine. Watu maelfu walikatwa mikono yao. Unyama ulisababisha watu kujitetea kwa silaha. Upinzani huu ulikandamizwa kwa ukali zaidi.

Kuna makadirio ya kwamba chini ya utawala wa Leopold idadi ya wakazi wa Kongo ilipungukiwa kutoka watu milioni 20 kubaki milioni 10 tu.

Upinzani didi ya Leopold hariri

Habari za unyama wa utawala wa Leopold ulienea kwa sababu wamisionari walipeleka barua na picha kwenda marekani na Ulaya. Tangu 1903 kamati za bunge la uingereza zilifanya utafiti kuhusu hali ya utawala wake Leopold. Upinzani ulikuwa pia ndani ya Ubelgiji na watu wengi waliona aibu kuhusu matendo ya mfalme wao.

Baada ya upinzani kukua mwaka 1908 Leopold alikabidhi Kongo kwa serikali ya Ubelgiji ikawa Kongo ya Kibelgiji.

Leopold alipokufa mwaka uliofuata watu barabarani walikashifu maiti yake ilipopita wakimwita aibu ya taifa.

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leopold II wa Ubelgiji kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.