Loyal to the Game ni jina la kutaja albamu ya nne kutolewa baada ya kifo cha hayati Tupac Shakur. Albamu ina maremixi kadhaa ambayo awali hayakutolewa na Tupac Shakur kabla ya kifo cha mnamo mwaka wa 1996. Albamu ilitolewa nchini Marekani mnamo tar. 14 Desemba 2004 (12 Desemba nchini Uingereza), Loyal to the Game ilitayarishwa na Eminem.

Loyal to the Game
Loyal to the Game Cover
Studio album ya 2Pac
Imetolewa 14 Desemba 2004
Imerekodiwa 1991-1994 (2Pac Vocals)
2004 (Production, Guest Vocals, etc.)
Aina Rap
Urefu 64:56
Lebo Amaru
Mtayarishaji Eminem, Scott Storch, DJ Quik, Red Spyda, Raphael Saadiq
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za 2Pac
2Pac Live
(2004)
Loyal to the Game
(2004)
Pac's Life
(2006)
Single za kutoka katika albamu ya Loyal to the Game
  1. "Thugs Get Lonely Too"
    Imetolewa: 2004
  2. "Ghetto Gospel"
    Imetolewa: 21 Agosti 2005

Kwa mujibu wa mahojiano yake na MTV, Eminem alivutiwa sana maisha ya Tupac na kazi zake na hivyo kumwandikia barua mama'ke Tupac, Afeni Shakur, akimwomba amruhusu kutayarisha albamu hii. Shakur amekubali, amempa Eminem haki za kuendelea kutayarisha albamu.[1] Albamu imetoa vibao vikali viwili - "Thugs Get Lonely Too" na "Ghetto Gospel".[2]

Eminem ametoa maujanja tofauti kadhaa wakati wa matayarisho ya albamu hii, amebadilisha hatua na uzito wa sauti ya Tupac ili iweze kwenda sawa na biti alizotayarisha.[3] Pia kumekuwa na matumizi mengi ya kukata na kubandika sauti ili kutengeneza maneno mapya yafofuatana na mwenendo wa utamaduni wa rap ya kisasa.

Ilifika kilele cha nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200 ikiwa na mauzo zaidi ya nakala 330,000 katika wiki yake ya kwanza. Halafu baadaye ilitunukiwa Platinum nchini Marekani na Dhahabu huko nchini Uingereza.[4]

Orodha ya nyimbo hariri

# Jina Watayarishaji Wageni walioshirikishwa Sampuli Muda
1 "Soldier Like Me (Return of the Soulja)" Eminem Eminem 3:50
2 "The Uppercut" Eminem E.D.I. na Young Noble 3:50
3 "Out on Bail" Eminem 3:54
4 "Ghetto Gospel" Eminem
  • Ina vionjo kadhaa kutoka katika wimbo wa "Indian Sunset" wa Elton John
3:58
5 "Black Cotton" Eminem Eminem, Kastro na Young Noble 5:03
6 "Loyal to the Game" Eminem G-Unit 3:23
7 "Thugs Get Lonely Too" Eminem Nate Dogg 4:48
8 "N.I.G.G.A. (Never Ignorant about Getting Goals Accomplished)" Eminem Jadakiss 3:02
9 "Who Do You Love?" Eminem 3:28
10 "Crooked Nigga Too" Eminem 2:55
11 "Don't You Trust Me?" Eminem Dido
  • Ina vionjo kadhaa kutoka katika wimbo wa "Do You Have a Little Time" wa Dido
4:55
12 "Hennessey" Eminem Obie Trice 3:27
13 "Thug 4 Life" Eminem 2:54
14 "Po Nigga Blues (Scott Storch Remix)" Scott Storch Ronald Isley 3:39
15 "Hennessy (Red Spyda Remix)" Red Spyda E.D.I. and Sleepy Brown 3:18
16 "Crooked Nigga Too (Raphael Saadiq Remix)" Raphael Saadiq 4:02
17 "Loyal to the Game (DJ Quik Remix)" DJ Quik DJ Quik & Big Syke 4:21

Nafasi za chati za albamu hariri

Mwaka Albamu Chati
Billboard 200 Top R&B/Hip Hop Albums Top Rap Albums Canadian Albums Chart
2004 Loyal To The Game #1 #1 #1 #7

Marejeo hariri

  1. "village voice > nyclife > The Essay: The End of Eminem by Jon Caramanica". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-22. Iliwekwa mnamo 2010-04-27. 
  2. Amazon.com: Loyal to the Game: 2Pac: Music
  3. "2Pac (Tupac Shakur) Loyal to the Game Lyrics Sounds and More". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-16. Iliwekwa mnamo 2010-04-27. 
  4. "vnu_content_id=1000741125 Tupac's 'Game' Haunts Album Chart At No. 1". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-27. Iliwekwa mnamo 2010-04-27.