Ludoviko wa Toulouse

(Elekezwa kutoka Ludoviko wa Anjou)

Ludoviko wa Toulouse (Brignoles, Provence, Ufaransa, Februari 1274 - Toulouse 19 Agosti 1297) alikuwa mwana wa mfalme wa Napoli Charles II wa Anjou, mdogo wake Ludoviko IX, lakini akitamani ufukara wa Kiinjili kuliko sifa na heshima za kidunia, alikataa haki ya kumrithi akawa mtawa wa Ndugu Wadogo na askofu wa Kanisa Katoliki mjini Toulouse[1].

Mt. Ludoviko wa Toulouse, katika mchoro wa Antonio Vivarini (1450), Louvre Museum.
Alivyochorwa na Piero Della Francesca.
Chombo cha fedha cha kutunzia masalia yake (Musée de Cluny).
Mt. Ludoviko wa Toulouse akiwa na nembo ya ukoo wake wa kifalme. (Hungarian Illuminated Chronicle).

Akiwa kijana kwa umri lakini mkomavu katika maadili alifariki mapema kutokana na afya wake dhaifu[2].

Alitangazwa na Papa Yohane XXII kuwa mtakatifu tarehe 7 Aprili 1317.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90385
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90385
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.