Ludoviko wa Casoria

Ludoviko wa Casoria, O.F.M. (Casoria, karibu na Napoli, 11 Machi 1814Posillipo, Napoli 30 Machi 1885), alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.

Alipata umaarufu kwa upendo mkubwa kwa maskini uliomfanya apambane na ufukara wa jamii na kwa kuanzisha mashirika mawili ya kitawa: Ndugu wa Kijivu wa Upendo na Masista wa Kijivu wa Mt. Elizabeti.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mwaka 1993, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Novemba 2014.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

  • Acta Ordinis Minorum (May, 1907), 156-158;
  • The Catholic World (November, 1895), 155-166;
  • Voce di Sant' Antonio (July, 1907), 23-26.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.