Luka wa Messina (Rossano, Calabria, karne ya 11 - Messina, Sicilia, 27 Februari 1149) alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Mashariki kwanza huko kwao, halafu karibu na mji huo akiwa abati wa monasteri aliyoianzisha mwenyewe katika kisiwa hicho.

Alijitahidi kurekebisha hali ya wamonaki wa mikoa hiyo miwili hata kwa kuwatungia sheria[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Februari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/43040
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

Kwa Kiitalia hariri

  • sac. Roberto Romeo, "Alle fonti del diritto liturgico orientale". Atti-Convegni-Ricerche ISSR - Messina. Anno 2011.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.