MV Bukoba ilikuwa feri iliyokuwa ikitoa huduma ya kubeba mizigo na abiria katika Ziwa Viktoria kati ya bandari za Bukoba na Mwanza[1].

Faili:MV Bukoba Memorial.jpg
Makumbusho kwa wahanga wa ajali ya MV Bukoba mjini Mwanza

Tarehe 21 Mei 1996 ilizama kwenye njia ya kuelekea Mwanza.[2] Abiria wengi walikufa na idadi yao imekadiriwa kuwa 1,000 hivi, lakini idadi iliyotangazwa rasmi ilikuwa 894[3].

Marejeo hariri

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/tujikumbushe-mv-bukoba-enzi-za-uhai-wake.1364063
  2. Lake Victoria tragedy ,Tanzania in May 21, kwenye tovuti ya asahi.net, iliangaliwa tar. 2 Desemba 2018
  3. The 13 Deadliest Shipwrecks Ever, tovuti ya gizmodo.com, iliangaliwa tar. 2 Desemba 2018