Mabilionea Ulimwenguni

Mabilionea Ulimwenguni ni orodha ya kila mwaka ya thamani ya utajiri ya mabilionea wakubwa duniani inayoandaliwa na kuchapishwa mwezi Machi kila mwaka na gazeti la Forbes la Marekani. Orodha ya kwanza ilichapishwa Machi 1987. Jumla ya thamani ya utajiri wa kila mmoja kwenye orodha hiyo unakadiriwa na kutolewa kwa dola ya Marekani kutegemeana na mali zao na madeni. Familia za Kifalme au madikteta ambao utajiri wao unatokana na nafasi zao na sio jasho huwa hawawekwi kwenye orodha hii.

Mwaka 2018, watu 2,208 wametokea kwenye orodha hii, ambayo ilijumuisha mabilionea wapya 259 wengi wao wakitokea China na Marekani, na watu 63 wenye umri chini ya 40 na wanawake 256.

Hadi 2018, mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates alikuwa ndio namba moja kwenye orodha hii kwa miaka 18 kati ya miaka 24, wakati mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos ameshika nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza na tajiri wa kwanza kwenye orodha mwenye utajiri thamani ya dola bilioni 100.[1] Mark Zuckerberg ni mtu pekee kwenye orodha ya mabilionea wakubwa 10 duniani mwenye umri wa chini ya miaka 50.[2]

Orodha ya kila mwaka hariri

Orodha huchapishwa kila mwaka mwezi Machi. Orodha hizi zinaonyesha mabilionea wakubwa 10 tu kila mwaka.

Maelezo hariri

Alama Maana
Haijabadilika toka mwaka uliopita.
  Imeongezeka toka mwaka ulliopita.
  Imepungua toka mwaka uliopita.

2019 hariri

Kwenye orodha ya Forbes ya 33, kuna mabilionea 2,153 ambao kwa ujumla wana thamani ya dola za Kimarekani trilioni 8.7.[3]

Na. Jina Thamani (USD) Umri Utaifa Chanzo cha utajiri
&0000000000000001.0000001 Bezos, JeffJeff Bezos $131 billion   55   Marekani Amazon
&0000000000000002.0000002 Gates, BillBill Gates $96.5 billion   63   Marekani Microsoft
&0000000000000003.0000003 Buffett, WarrenWarren Buffett $82.5 billion   88   Marekani Berkshire Hathaway
&0000000000000004.0000004 Arnault, BernardBernard Arnault $76 billion   70   Ufaransa LVMH
&0000000000000005.0000005   Slim, CarlosCarlos Slim $64 billion   79   Meksiko América Móvil, Grupo Carso
&0000000000000006.0000006 Ortega, AmancioAmancio Ortega $62.7 billion   82   Hispania Inditex, Zara
&0000000000000007.0000007   Ellison, LarryLarry Ellison $62.5 billion   74   Marekani Oracle Corporation
&0000000000000008.0000008   Zuckerberg, MarkMark Zuckerberg $62.3 billion   34   Marekani Facebook
&0000000000000009.0000009   Bloomberg, MichaelMichael Bloomberg $55.5 billion   77   Marekani Bloomberg L.P.
&0000000000000010.00000010   Page, LarryLarry Page $50.8 billion   45   Marekani Alphabet Inc.

Marejeo hariri

Specific
  1. Kroll, Luisa. "Forbes 2017 billionaires list: Meet the richest people on the planet", Forbes. 
  2. Shinal, John (2017-08-01). "Mark Zuckerberg is less than half the age of his super-wealthy peers". www.cnbc.com. Iliwekwa mnamo 2019-01-15. 
  3. "Billionaires 2019". Forbes. 5 March 2019. Iliwekwa mnamo 13 March 2019.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

Viungo vya nje hariri