Madelberta (pia: Madelberte, Machtelberthe; Ufaransa karne ya 7 - Maubege, leo nchini Ufaransa, 705 hivi) alikuwa bikira aliyeongoza monasteri ya Maubege kama abesi chini ya kanuni ya Kolumbani kuanzia mwaka 697 baada ya dada yake, Aldetruda.

Mt. Madelberta alivyochorwa.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Septemba[1].

Familia hariri

Mtoto wa wazazi wa koo mashuhuri, Visenti Madelgari na Vatrude, alikuwa mdogo wa Landeriki, Dentelini na Adeltruda, ambao wote watano ni watakatifu pia [2].

Tanbihi hariri

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  • Bertrand, Paul, mhr. (1997), "La Vie de Sainte Madelberte de Maubeuge", Analecta Bollandiana (Text (BHL 5129) and French translation), 115 (1–2), doi:10.1484/J.ABOL.4.01703
  • Butler, Alban (1866), The Lives of the Fathers, Martyrs, and Other Principal Saints, James Duffy, iliwekwa mnamo 2021-07-26
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.