Majadiliano:Kidudu mtu

Latest comment: mwaka 1 uliopita by ChriKo in topic Makala yenye mashaka

Makala yenye mashaka hariri

Makala haiwezi kubaki jinsi ilivyo. Haina habari halisi kuhusu mdudu yule. Kama watu katika eneo fulani kweli wanatumia jina hilo kwa mdudu fulani, basi hatupewi habari za kutosha kumwelewa mdudu. Hakuna vyanzo vyovyote. Iboreshwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 14:05, 17 Desemba 2022 (UTC)Reply

Wengi wamemuona, ila hawajui jina la kisayansi. Tuombe msaada wa ChriKo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:56, 17 Desemba 2022 (UTC)Reply
Ndiyo, watu wengi wamemwona na kadhaa wamenitumia picha. Lakini picha hizi hazifanani na picha ya makala. Zaidi ya hayo, "apefly" hapatikani Afrika ya Mashariki, isipokuwa amevamia hapa hivi karibuni. Mnakubali nifute makala hii? Taarifa yake si sahihi. ChriKo (majadiliano) 13:38, 18 Desemba 2022 (UTC)Reply
Je, huwezi kuisahihisha? Maana watu wanazungumzia sana mdudu huyo na wanahitaji kujua ukweli. Wilaya ile imetoa taarifa iliyotumiwa na Kipala, lakini labda si sahihi. Tunaomba uifanyie kazi. Shukrani! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:41, 18 Desemba 2022 (UTC)Reply
Samahani! Sasa nimechimba zaidi kidogo. "Apefly" haipatikani katika Afrika, lakini "African apefly" anapatikana. Kuna spishi mbili nchini Tanzania, lakini ni spishi moja tu iliyoenea sana. Tudhani kuwa ni spishi hiyo. ChriKo (majadiliano) 14:22, 18 Desemba 2022 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Kidudu mtu ".