Majadiliano:Windhoek

Oliver, nimebadilisha picha kidogo (usipopenda basi rudisha hali ya awali) ili nikuonyeshe mambo machache ilhali wewe ni mgeni:

a) ukinakili picha na ukitaka maandishi yaonekane pamoja na picha: basi hakikisha ya kwamba |thumb| iko mara baada ya jina la picha yenyewe >> Image:Windhoek-Skyline.jpg|thumb|. Amri hii inasababisha mraba uonekane pamoja na nafasi ya maandishi.Maelezo ni mwisho kabisa. Nimeweka sasa "|Kitovu cha mji wa Windhoek"

b) angalia unataka mwelekeo gani: left - center - right

c) kuweka viungo : ukifungua makala tuseme ya Kiingereza - boyeza edit (kama ukitaka kuazima picha na kunakili mstari wake) - nenda mwishoni kabisa - utaona orodha ya viungo: af:Windhoek ar:ويندهوك da:Windhoekde:Windhuk na kadhalika.

sasa unanakili viungo vya lugha nyingine na kupachika katika makala yako mwisho kabisa.

Unaweza kuongeza shughuli mbili: a) mara umeshafungua Kiingereza/edit basi weka mstari mpya baada ya "k" na ingiza kiungo chako kipya yaani "sw:Windhoek" halafu weka [[ ]]

b) katika makala yako Kiingereza haimo (kwa sababu umenakili pale) kwa hiyo unafanya mstari mpya kwenye "e" na kuingiza "en:Windhoek" halafu [[ ]]

Naona si vigumu hata usipojisikia mtaalamu wa mitambo nimeshaone unajifunza haraka sana - kwa maswali mengine mimi humwuliza Matt Crypto au Marcos. --Kipala 13:44, 2 May 2006 (UTC)

Return to "Windhoek" page.