Majiji yasiyoonekana

Majiji yasiyoonekana (kwa Kiitalia "Le città invisibili", na kwa Kiingereza "Invisible Cities") ni kitabu cha hadithi kilichoandikwa na mwandishi toka Italia, Italo Calvino.

Kitabu hiki kinaelezea mazungumzo kati ya msafiri Marco Polo kutoka mji wa Venice, Italia, na mfalme wa Mongolia, Kublai Khan.

Kitabu kimeandikwa kwa mtindo wa pekee kwani hakina mfumo uliozoeleka wa vitabu vya fasihi: mwanzo, katikati, mwisho. Ndani ya kitabu hiki wahusika wanaotambulika ni wawili tu, Kublai Khan na Marco Polo.

Kublai Khan alikuwa akifurahi sana kusikia visa toka kwa Marco Polo. Visa toka kwa wakazi wa ufalme wake vilikuwa vinamchosha. Khan alitaka sana Marco Polo aongelee juu ya mji alikozaliwa, Venice, lakini Marco Polo alipendelea kuongelea miji ya kufikirika na kusadikika.

Kitabu hiki kina visa 55 vinavyoelezea miji hiyo ya kufikirika na kusadikika pamoja na mazungumzo ya kifalsafa kati ya Khan na Polo.

Moja ya mazungumzo yanayojulikana sana ni lile kuhusu jiwe na daraja. Marco Polo alimpa Kublai Khan uchambuzi wa daraja ni nini akielezea jiwe hata jiwe. Kublai Khan akauliza, "Je ni jiwe lipi linaloshikilia daraja?" Marco Polo akajibu, "Hakuna jiwe moja linaloshikilia daraja, si jiwe hili wala lile bali mhimili ambao mawe hayo yameujenga kwa pamoja."

Kublai akakaa kimya kwa muda akifikiri, kisha akasema, "Basi sitaki kusikia kuhusu mawe, nataka uniambie kuhusu huo mhimili." Marco Polo akajibu, "Bila mawe hakuna mhimili."

Kati ya miji ya kufikirika na kusadikika iliyoelezewa ndani ya kitabu hiki baadhi ni: mji ambao wakazi wake wanatupa vitu vyao vyote kila siku na kununua vitu vipya, mji wa wafu ulio chini ya ardhi, na mji uliojengwa na watu waliomuona mwanamke uchi ndotoni kisha akatokomea (watu hawa waliamua kujenga mji ambao barabara zake zinaelekea kule alikoelekea huyo mwanamke waliyemuona ndotoni na wakajenga kuta ili kumzuia asiweze kutoroka akitokea tena.)

Majiji makubwa ya dunia hariri

Leo hii kuna majiji 20 yenye wakazi zaidi ya milioni 10:

Viungo vya Nje hariri