Malaika mkuu (kwa Kigiriki ἀρχάγγελος arkh- + angelos)[1]ni jina la heshima kwa baadhi ya malaika wenye hadhi ya juu kati ya viumbe vya kiroho.

Mchoro wa Guido Reni ukionyesha ushindi wa malaika mkuu Mikaeli dhidi ya Shetani, 1636.

Msingi wa imani hiyo ni kwamba kila malaika ameumbwa peke yake na tofauti na wengine wote, na kwamba katika kumtumikia Mungu aliyewaumba wanashirikiana kwa ngazi.

Biblia ya Kikristo inatumia jina hilo mara mbili: katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike 4:16 na katika Waraka wa Yuda 1:9, ambapo linamhusu malaika Mikaeli.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.