05°00′S 39°03′E / 5.000°S 39.050°E / -5.000; 39.050

Kwa ndani.

Mapango ya Amboni ni mapango makubwa ya chokaa katika Afrika Mashariki. Yanachukua nafasi ya km2 234.

Mapango hayo yako kaskazini kwa mji wa Tanga nchini Tanzania, kilomita 8 kwa njia ya barabara ya Tanga-Mombasa.

Mapango hayo yaliundwa karibu miaka milioni 150 iliyopita wakati wa Jurassic. Kulingana na watafiti eneo hilo lilikuwa chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita.

Kuna mapango kumi lakini moja tu hutumiwa kwa ziara za kuongozwa.

Picha hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri