Maporomoko ya Kalambo

Maporomoko ya Kalambo yanatokana na mto Kalambo ambao ni mpaka wa Tanzania na Zambia.

Maporomoko ya Kalambo

Maporomoko ya maji hayo, ukiachilia kuwa ni ya pili baada ya yale ya Tugela (Afrika ya Kusini), lakini pia ndiyo maporomoko pekee yanayogawa nchi mbili.

Maporomoko hayo yapo katika kijiji cha Kapozwa, kata ya Kisumba, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa. Katika kijiji cha Kapozwa, ambacho kilianzishwa kutokana na imani kuwa ukienda kuoga katika maporomoko hayo utapooza. Kwa kuambiwa hivyo wenyeji wa eneo hilo walipaita kijiji jina la Kapozwa.

Maporomoko hayo yamekuwa yakionekana na kutangazwa kuwa yapo Zambia na hivyo kuiondoa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye maporomoko yanayotambulika duniani.

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri