Mary Douglas Nicol Leakey (London, 6 Februari 1913 - Nairobi, 9 Desemba 1996) alikuwa mtaalamu wa akiolojia aliyepata kuwa maarufu kutokana na kukuta ushuhuda juu ya maendeleo ya zamadamu.

Mary Leaky

Alikuta na kutambua fuvu fosili ya kwanza ya sokwe mkubwa kwenye kisiwa cha Rusinga na baadaye aina ya sokwe iliyofanana zaidi na binadamu iliyoitwa Zinjanthropus kwenye bonde la Olduvai. Alikuta pia nyayo za Laitoli zilizo kati ya ushuhuda wa kale kabisa wa viumbehai waliotembea kwa kutumia miguu miwili tu.

Tangu mwaka 1960 alikuwa mkurugenzi wa uchimbaji huko Olduvai. Baada ya kifo cha mumewe Louis aliendelea kuwa kati ya wataalamu wakuu kwenye uwanja wa paleoanthropolojia akamfundisha pia mwanawe Richard Leakey katika fani hii.

Viungo vya nje hariri