Masadukayo (kwa Kiebrania צדוקים sadukim) waliunda madhehebu muhimu ya dini ya Uyahudi wakati wa Yesu Kristo. Walikuwa na nguvu hasa kati ya makuhani waliohusika na matukio ya hekalu, htifaki, taratibu za dini, na liturujia. Ndiyo maana waliishiwa nguvu hekalu la Yerusalemu lilipoangamizwa na Warumi pamoja na mji mzima mwaka 70 B.K.

Walikubali Torati ya Musa tu, na kukataa vitabu vingine vyote vya Biblia. Kwa msingi huo, walikataa mafundisho yaliyoletwa na manabii, kama vile juu ya ufufuo wa wafu [1] na uzima wa milele [2]. Katika hilo waligongana na Mafarisayo na Yesu ambaye, kadiri ya Injili, ndio waliohusika zaidi na kifo chake.

Vilevile, walikanusha uwepo wa malaika [3] Tena, walichukulia "jino kwa jino" (yaani, lex talionis) kiuhalisi na waliunga mkono adhabu za kimwili ikiwemo adhabu ya kifo (badala ya mapatano ya kifedha)

Mvutano mwingine kati ya madhehebu hayo ulizuka kutokana na ukweli kwamba Masadukayo waliwakilisha daraja la kijamii na umiliki wa ardhi. Hawa walikuwa wenye mamlaka (Antiquities 13.10.6; 18.1.4-5; 20.9.1), ambapo Mafarisayo na waandishi walikuwa wasomi na wacha Mungu miongoni mwa watu. Mvutano huu ungeweza kubainishwa kama hekalu la Yerusalemu dhidi ya masinagogi yaliyoenea kote.

Marejeo hariri

  1. Math 22:23; Mk 12:18; Lk 20:27; Mdo 4:1-2; 23:8
  2. Marko 12:18; Yosefu Flavius, Antiquities 18.1.3-4; Wars 2.8.14
  3. Mdo 23:8
  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Masadukayo kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.