Mauritania ni nchi ya Afrika kaskazini-magharibi. Upande wa magharibi kuna pwani ya bahari ya Atlantiki, upande wa kusini imepakana na Senegal, upande wa mashariki na Mali na Algeria, upande wa kaskazini na Sahara ya Magharibi inayotawaliwa na Moroko.

Mauritania

Jina limeteuliwa kutokana na Mauritania ya kale iliyokuwa ufalme wa Waberber kusini kwa Mediteranea katika eneo la Algeria na Moroko ya leo.

Mji mkuu ni Nouakchott. Mji wa pili na kitovu cha uchumi ni bandari ya Nouadhibou karibu na mpaka wa Sahara Magharibi.

Wilaya za Mauritania hariri

Mauritania ina wilaya 12 (zinaitwa "wilāyah").

  1. Adrar (Atâr)
  2. Assaba (Kifa)
  3. Brakna (Aleg)
  4. Dakhlet Nouâdhibou (Nouâdhibou)
  5. Gorgol (Kaédi)
  6. Guidimaka (Sélibabi)
  7. Hodh ech Chargui (Néma)
  8. Hodh el Gharbi (‘Ayoûn el ‘Atroûs)
  9. Inchiri (Akjoujt)
  10. Nouakchott (mji mkuu)
  11. Tagant (Tidjikja)
  12. Tiris Zemmour (Zouérat)
  13. Trarza (Rosso)
 

Siasa ya Mauritania hariri

Mnamo Machi 2007 wananchi walipata nafasi ya kumchagua rais mara ya kwanza katika historia ya nchi tangu uhuru. Sidi Ould Cheikh Abdallahi alishinda katika duru ya pili kwa 53% za kura zote akaapishwa tarehe 20 Aprili 2007.

Watu hariri

Wakazi wengi (70%) ni Wamori, mchanganyiko wa Waarabu, Waberber na Waafrika waliotokana na watumwa kutoka kusini kwa Sahara. Asilimia 30 zilizobaki ni makabila ya Kiafrika yasiyoongea Kiarabu, ambacho ndicho lugha rasmi.

Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu (hasa Wasuni). Uhuru wa dini unabanwa sana kwa nyingine zote.

Pamoja na hayo, hadi leo asilimia 4 za wakazi ni watumwa, ingawa mwaka 2007 ilifutwa haki ya kuwamiliki.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mauritania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.