Mena wa Misri (pia: Menna, Menas, Minas, Mina; Nikiou, 285-309 hivi) alikuwa askari Mkristo aliyeuawa kwa ajili ya imani yake karibu na ziwa Maryut.

Yesu na Mena, picha takatifu ya karne ya 6 kutoka Bawit, Misri ya Kati, moja kati ya zile za kale zaidi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[1].

Jinsi alivyoheshimika kutokana na miujiza iliyofanyika kwenye kaburi lake, juu yake umeanzishwa mji (Karm Abu Mina) ulioorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.