Michael Mike Okoth Origi (alizaliwa 16 Novemba 1967) ni mchezaji wa zamani wa kandanda kutoka nchi ya Kenya. Wakati mwingi wa wasifu wake, alisakata kabumbu ya utaalamu nchini Ubelgiji.

Wasifu hariri

Origi alianza wasifu wake kwa kuvichezea vilabu vya Shabana na Kenya Breweries (sasa Tusker FC) nchini Kenya. Mnamo mwaka wa 1992 alihamia klabu iliyoko nchini Omani inayojulikana kama Boshar FC na miezi mitatu baadaye akahamia klabu ya KV Oostende nchini Ubelgiji. Msimu wake uliyokuwa na mafanikio zaidi ulikuwa ule wa 1998/1999, wakati klabu yake ya Racing Genk ilishinda taji la ligi ya Jupiler ambayo ni ligi ya divisheni ya kwanza ya Ubelgiji. Mnamo mwaka wa 2006, akiwa na umri wa miaka 38, akiwa bado hodari, alikuwa anasakata kabumbu katika ligi lakini ya divisheni ya chini.

Kimataifa hariri

Origi alikuwa mchezaji wa mara kwa mara ya wa timu ya kandanda ya kitaifa ya Kenya na alicheza katika Kombe la Mataifa ya Afrika mara tatu (1990, 1992 na 2004).

Maelezo mengine. hariri

Mike Origi alikuwa anajulikana nchini Ubelgiji kwa kuwa mwanakandanda mwungwana , kamwe hakulalamika, kamwe hakupinga uamuzi wa refari na kamwe hakumpa jeraha mpinzani wake. Miongoni mwa mashabiki alikuwa anajulikana kwa kuwa urafiki wake na hali yake ya kuwa mtu wa 'kawaida'.

Vilabu & misimu hariri

  • Shule ya Upili ya Itierio
  • Shabana Kisii (kama mlinda lango )
  • Kenya Breweries -1992
  • Boshar FC 1992 (Miezi 3)
  • Oostende KV 1992/1993 - 27, 8
  • Oostende KV 1993/1994 - 16, 0
  • Oostende KV 1994/1995 - 13, 2
  • Oostende KV 1995/1996 - 15, 1 (Divisheni ya II)
  • KRC Harelbeke 1996/1997 - 27, 5
  • KRC Harelbeke 1997/1998 - 29 6
  • Racing Genk 1998/1999 - 32, 12
  • Racing Genk 1999/2000 - 23, 6
  • Racing Genk 2000/2001 - 23, 2
  • Racing Genk 2001/2002 - 2, 0 - Alihamia Molenbeek mnamo Januari mwaka wa 2002
  • RWD Molenbeek 2001/2002 - 25, 10
  • Heusden Zolder 2002/2003 - 0, 0 (Divisheni ya II)
  • Heusden Zolder 2003/2004 - 30, 3
  • KSK Tongeren 2004/2005 - 28, 15 (Divisheni ya III)
  • SK Tongeren 2005/2006 - 27, 10 (Divisheni ya III)
  • Cobox 76 2006-2007 (Divisheni ya V: Kiwango cha I cha Mkoa)

Kibinafsi hariri

Kakake Austin Oduor Origi pia alikuwa mchezaji kandanda na aliichezwa klabu ya Gör Mahia, huku ndugu yake mwingine Gerald Origi aliamua kucheza katika safu ya ulinzi katika klabu ya Kenya Breweries (sasa Tusker FC) katikati ya miaka ya 1990. Kakake mwingine, Anthony Origi pia alikuwa mchezaji wa safu ya ulinzi katika klabu ya Tusker. Mwananwe Austin, Arnold Origi Otieno ni mlinda lango na alikuwa mlinda lango wa kitambo wa Tusker F.C. kabla ya kujiunga na klabu ya Ulaya. Arnold pia ni mlinda lango wa timu ya kandanda ya kitaifa ya Kenya.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Mchezaji Soka wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mike Okoth Origi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.