Mitume na Manabii katika Uislamu

Manabii wa Uislamu ni binadamu wanaume ambao huhesabiwa na Waislamu kuwa manabii waliochaguliwa na Mungu. Kwa imani ya Kiislamu manabii hao wote walihubiri ujumbe uleule wa kumwabudu Allah.

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Kwenye Qur'an

Kuna majina ya watu 25 kwenye Qur'an wanaotajwa kuwa manabii. Wengi kati yao hutajwa pia katika Biblia na majina yao jinsi yalivyo kawaida katika Uyahudi na Ukristo yanatajwa katika mabano.

Sehemu za habari za manabii wa Qurani na watu wa Biblia hulingana, lakini mara nyingi ziko tofauti pia. Kwa mfano Ibrahim wa Qurani aliambiwa na Mungu kumtoa mwanawe kama sadaka lakini jina lake halitajwi, kumbe katika Biblia habari hii inasimuliwa juu ya Isaka. Dawud hutajwa na Qurani kama nabii, wakati Daudi wa Biblia ni mfalme mwenye manabii wake (hasa Gad na Nathan), ingawa anaweza kuhesabiwa kama nabii kwa sababu ya kuchangia kitabu cha Zaburi (ambacho kina utabiri mbalimbali kuhusu Yesu.

Manabii hao wa Qurani ni pamoja na
(jina la Qurani, kwa maandishi ya Kiarabu,, sura ya Qurani anapotajwa, jina la Kibiblia linaloweza kumaanishwa)

  1. Adam (آدم , Sura 3:33 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Adamu)
  2. Idris au Idrisa (إدريس, Sura 19:54 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Henoko)
  3. Nuh (نوح, Sura 26:10 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine. ) (Nuhu)
  4. Hud (هود, Sura 26:125 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine. ) (labda Eberi),
  5. Saleh au Salih (صالح, Sura 26,143 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (labda Shilo wa Biblia)
  6. Ibrahim au Ibrahimu (إبراهيم, Sura 9,70 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Abrahamu)
  7. Luut (لوط, Sura 26,162 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Lut)
  8. Ismail au Ismaili (إسماعيل, Sura 19,54 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Ishmaeli)
  9. Ishaq au Isihaka (إسحاق, Sura 19,49 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Isaka)
  10. Ya'qub au Yakubu (يعقوب, Sura 19,49 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Yakobo Israeli)
  11. Yusuf (يوسف, Sura 6:89 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Yusufu)
  12. Ayyub (أيوب, Sura 6,89 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Ayubu)
  13. Shu'aib (شعيب, Sura 24,178 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Yethro)
  14. Musa (موسى, Sura 19,51 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Musa)
  15. Harun au Haruni (هارون, Sura 19,53 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Aroni)
  16. Dzul-Kifli (ذو الكفل, Sura 38,48 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (labda Ezekieli
  17. Dawud (داود, Sura 6,89 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Daudi)
  18. Suleyman au Suleimani (سليمان, Sura 6,89 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Solomoni)
  19. Ilyas au Ilyasa (إلياس, Sura 37,173 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (labda Eliya)
  20. Al-Yasa (اليسع, Sura ) (Elisha)
  21. Yunus (يونس, Sura 6,89 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (nabii Yona)
  22. Zakariyya (زكريا 6,89 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Zakaria)
  23. Yahya (يحيى, Sura 3,39 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Yohane Mbatizaji)
  24. Isa (عيسى, Sura 4,171 Archived 29 Januari 2009 at the Wayback Machine.) (Yesu)
  25. Muhammad

Mitume na Manabii

Kufuatana na mafundisho ya Uislamu katika dini zote za mbinguni ambazo Mwenyezi Mungu amewaletea wanadamu kwa njia ya Mitume na Manabii, kama dini ya Kiyahudi, dini ya Kinasara (Ukristo) na dini ya Kiislamu, hao Mitume na Manabii wametajwa katika vitabu walivyokuja navyo, na hii ni ishara moja kubwa kuwa dini hizo zina asili moja na Mwenyezi Mungu mmoja.

Mitume katika Talmud

Katika kitabu cha Wayahudi cha Talmud, Mitume wao wametajwa kama ifuatayo:

Abrahamu, Isaka, Yakobo, Mose, Haruni, Yoshua, Samueli, Solomoni, Obadia, Jehu bin Hanani, Azaria bin Odedi, Jahazieli Mlawi, Eliezeri bin Dodavahu, Hosea, Amos, Mika, Amoz (baba wa nabii Isaya), Eliya, Elisha, Yona, Isaya, Yoeli, Nahumu, Habakuki, Sefania, Uria, Yeremia, Ezekieli, Shemaia, Baruku, Neria (baba wa Baruku, Meseia (baba wa Neria), Hagai, Zekaria, Malaki yaani Ezra, Hasofer, Mordekai Bilshan, Oded (baba wa Azaria), na Hanani (baba wa Jehu)

Mitume wengine katika Biblia

Mitume wengine walitajwa katika Agano la Kale, kati yao ni: Adamu, Noah (Nuh), Yuda (Yahuda), Daudi.

Wengine tena wanatajwa katika Agano Jipya, hasa Yohane Mbatizaji (Yahya) na Yesu bin Mariamu ('Îsa).

Mitume katika Qurani

Mwenyezi Mungu ametaja Mitume na Manabii 25 katika Qurani, na katika Hadithi za Mtume Muhammad imetajwa kuwa idadi yao kwa jumla ni 124,000, katika hao 315 ni Mitume na waliobaki ni Manabii.

Kati ya hao waliotajwa ndani ya Qurani ni:

Adam, Idris, Nuh, Hud, Salih, Lut, Ibrahim, Ismail, Is-haq, Yaqub, Yusuf, Shu'aib, Ayyub, Dhulkifl, Musa, Harun, Daud, Sulaiman, Ilyas, Ilyas'a, Yunus, Zakaria, Yahya, Isa, na Muhammad.

Miongoni mwao, watano ni Mitume wakubwa ambao walipewa mitihani mingi wakawa na subira kustahimili matatizo ya umma zao. Hawa ni Nuhu, Ibrahimu, Musa, Isa na Muhammad.

Tofauti baina ya Mitume na Manabii

Mitume ni wale ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa kauma na umma mbalimbali ili kuwaelekeza njia yake na kuwaepusha na njia za upotofu za Ibilisi na Shetani.

Kumbe Manabii ni wale walioletewa ufunuo na wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili wawafahamishe watu wao kuhusu ujumbe wake.

Lakini si wote wanakubali kuwatofautisha hivyo.

Ujumbe wa Mitume na Manabii

Kadiri ya Uislamu Mitume na Manabii wote, tangu alipoletwa Adam mpaka Mtume wa mwisho kuletwa duniani, wote wamekuja na ujumbe mmoja wa kuwa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote na viumbe vyote ni Mmoja na hana mshirika, na kuwa yeyote atakayemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, basi huyo huwa amepotea na ametoka njia iliyonyoka, na malipo yake ni kutiwa motoni milele.

Marejeo

  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.