Mkondo wa Atlantiki ya Kaskazini

Mkondo wa Atlantiki ya Kaskazini ni jina la sehemu ya kaskazini ya "mkondo wa Ghuba".

Mkondo wa Ghuba - sehemu ya kaskazini ni Mkondo wa Atlantiki ya Kaskazini

Mkondo huu katika bahari hutokea katika ghuba ya Meksiko na kuvuka Atlantiki. Kabla ya kufika funguvisiwa ya Britania unajigawa katika mikono miwili. Mkono wa kaskazini huitwa "Mkondo wa Atlantiki ya Kaskazini".

Hupeleka maji ya vuguvugu kutoka kusini kwenda kaskazini na kuwa na athari kubwa kwa hali ya hewa hasa ya Ulaya.

Kwa njia hi hali ya hewa ya Ulaya ya kaskazini na magharibi si baridi jinsi ilivyo katika Amerika kwenye latitudo ileile. Joto linalokuja na maji ya mkondo huzuia baridi kali. Maji ya mkondo wa ghuba husababisha mabandari ya Ulaya ya Kazkazini hadi Murmansk kuwa bila barafu hata wakati wa baridi.

Hali ya hewa ya Ulaya inaruhusu kustawi kwa mazao ya kutosha ya kulisha watu wengi - wakati huohuo maeneo ya Kanada katika latitudo ileile hazina watu kutokana na vipindi virefu vya baridi. Katika Kanada kwenye latitudo ya 60 hakuna miti tena kwa sababu ya kipindi kirefu cha baridi - katika Ulaya miji ya Sankt Petersburg, Helsinki, Stockholm na Oslo iko kwenye latitudo ileile.