Mnana
Mnana tumbo-dhahabu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Jenasi: Ploceus
Cuvier, 1816
Ngazi za chini

Spishi 10:

Minana ni ndege wadogo wa jenasi Ploceus katika familia Ploceidae ambao wanatokea Afrika. Wanafanana na kwera lakini hawana nyeusi kichwani. Ndege hawa hula mbegu hasa lakini wadudu pia, hususa makinda. Hulifuma tago lao kwa majani ya manyasi na hulining'inizia kitawi. Matago yao hupatikana katika makundi makubwa. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi hariri

Picha hariri