Mtini
(Ficus carica)
Mtini
Mtini
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Rosales (Mimea kama mwaridi)
Familia: Moraceae (Mimea iliyo na mnasaba na mforosadi)
Jenasi: Ficus
Röding
Spishi: F. carica
L.

Mtini (Ficus carica) ni mti mkubwa, kama kichaka au mdogo wenye asili ya kusini magharibi mwa Asia na pande za mashariki mwa Mediteranea (kutoka Afghanistani mpaka Ugiriki). Huwa na kimo cha mita 6.9 mpaka 10, na shina laini la kijivu. Majani yana urefu wa sm 12-15 kwa urefu na sm 10 -18 kwa upana, yakiwa yamegawanyika katika vipande vitatu au vitano. Matunda yake, matini huwa na urefu wa sm 3-5 na ngozi ya kijani, wakati mwingine huwa na kuwa ya zambarau au kahawia. Majimaji ya tini huwasha ngozi ya binadamu.

Kilimo matumizi, mtini hulimwa kwa ajili ya matunda yake yanayoliwa kwanzia sehemu za asili za Mediteranea, Irani na kaskazini mwa Uhindi. Pia hupatikana maeneo haya hasa huko Marekani, Mexiko, Chili, Australia na Afrika Kusini. Matini hupatikana pia kwenye maeneo ya joto, kama Hansari, na huchumwa mara mbili au tatu kwa mwaka. Tunda hili limekuwa chakula kwa watu wengi kwa miaka zaidi ya elfu na liliaminika kuwa vina virutubisho. Tini inayoliwa ni miongoni mwa mimea ya mwanzo kabisa na binadamu kwaajili yakula kwa mabaki tisa ya tini yanayoonyesha yalikuwepo 9400-9200 KK. Pengine hata mawazo ya kilimo ndio yalikuwa ndo yanaanza wakati huo na husemwa kwamba mimea mingi kama vile ngano, shairi nk.

Tini pia kilikuwa chanzo kizuri cha chakula kwa Waroma, tini kulikuwa kama zilivyoau baada ya kukaushwa na hutumika kutengenezea jamu. Tini inayouzwa mara nyingi huwa katika mtindo wa kukaushwa, sabsbu tini ikiisha kuwa huwa vigum kusafirishwa na haiwezi kudumu kwa muda mrefu baada ya kuchumwa.


Uzalishaji hariri

Kulingana na taarifa za FAO, uzsalishaji wa tini kwa mwaka 2005 ulikuwa tani 1,057,000. Utumizi ikifatiwa na misri tani 170,000 na nchi nyingine za mediterania.


Tini na Afya hariri

Tini ni moja ya mimea yenye kiasi kikubwa cha kalisi na makapi. Tini iliyokaushwa kuwa na kiasi kikubwa cha makapi, shaba, manganisi, magnesi, kali, kalisi na vitamini K, kulingana na mahitaji ya binadamu. Huwa na kiwango kidogo cha virutubisho vingine. Katika tafiti moja, gram 40 tu za tini iliyokaushwa kuongeza uwezo kwa kiasi kikubwa cha plazma antioksidanti mwilini.

Picha hariri