Mtori (shukrabenedic)

Mtori ni chakula maarufu nchini Tanzania kinachotengenezwa kwa kutumia ndizi na nyama, lakini pia huweza kuwa na viambato vingine ndani yake (kama vile viazi, maziwa au kream)[1]. Chakula hiki asili yake ni kutoka katika eneo la mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania, hasa eneo la Wilaya ya Moshi na mkoa wa Arusha[2].

Ndizi au ndizi za kijani mara nyingi huliwa katika eneo hili kama chanzo kikuu cha wanga[1]. Tangu wakati huo aina hii ya chakula imeenea katika maeneo mengine kote nchiniTanzania[3]. Katika utengenezaji wa Mtori, Kijadi fimbo maalum hutumiwa kusaga ndizi[2]. Mtori mara nyingi huliwa na wanawake wa Kimasai katika kipindi cha miezi mitatu baada ya kujifungua kwa ajili ya lishe[4]. Katika kipindi hiki cha baada ya kujifungua, wanawake hupewa hasa vyakula laini (laini) kula kama mtori[5].

Kwa sababu ni chakula chenye nguvu, kinaweza kutumiwa kama chakula kuu[6]. kinaweza kuliwa wakati wa kifungua kinywa, chakula cha mchana, au chakula cha jioni[1].

Marejeo;

  1. 1.0 1.1 1.2 Kitu Kizuri (kwa Kiingereza). Kitu Kizuri LLC. 2008. 
  2. 2.0 2.1 Riyamy, Alya Sened (2001). African Gardens: The Cuisine of Zanzibar and the East African Coast (kwa Kiingereza). Riyamy Publications. 
  3. Gall, Timothy L.; Hobby, Jeneen (2009). Worldmark Encyclopedia of Cultures and Daily Life: Africa (kwa Kiingereza). Gale. ISBN 978-1-4144-4883-1. 
  4. Horn, Corinna (2013-09-16). Maasai Cooking (kwa Kiingereza). Books on Demand. ISBN 978-3-7322-8040-7. 
  5. Seura, Suomen Antropologinen (1999). Shifting Ground and Cultured Bodies: Postcolonial Gender Relations in Africa and India (kwa Kiingereza). University Press of America. ISBN 978-0-7618-1388-0. 
  6. Webb, Lois Sinaiko (2000). Multicultural cookbook of life-cycle celebrations. Internet Archive. Phoenix, AZ : Oryx Press. ISBN 978-1-57356-290-4.