Mtumiaji:Dee Soulza/Imani (Uislamu)

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya
Uislamu na Imani

Aina za watu

'Muuminianayesadiki 'Mwislamuanayejinyenyekeza [kwa Allah] Mpotovudhahiri mwenye dhambi, fisadi Mwovumwenye dhambi (kwa matendo) Kafirimkataa Uislamu (asiye Mwislamu) Mnafikindumilakuwili

Makundi

Ahl al-Kitâb

Ahl al-Fatrah

Msamiati
Dini

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya
Uislamu na Imani

Aina za watu

'Muuminianayesadiki 'Mwislamuanayejinyenyekeza [kwa Allah] Mpotovudhahiri mwenye dhambi, fisadi Mwovumwenye dhambi (kwa matendo) Kafirimkataa Uislamu (asiye Mwislamu) Mnafikindumilakuwili

Makundi

Ahl al-Kitâb

Ahl al-Fatrah

Msamiati
Dini

Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu Uislamu

ImaniMungu hana mshirika

Malaika

Vitabu vilivyobainishwa

Mitume

Siku ya Ufufuo

Mungu ndiye mpangaji wa yote.

Mambo ya kutendwa

Kada ya Imani

Sala (swala)

Kutoa dhaka

Imani (Kwa Kiarabu hutamkwa: īmān) na maana yake kwa Kiswahili ni imani au utambuzi wa kiimani. Katika theolojia ya Kiislamu inaashiria hali ya muumini wa Kiislamu kuupokea Uislamu na misingi yake yote . [1] [2] Ufafanuzi wake rahisi zaidi ni kuamini katika nguzo kuu sita za imani, zinazojulikana kama arkān al-īmān .

Neno Imani limefafanuliwa katika Kuruani na Hadithi. Kwa mujibu wa Kuruani, iman lazima iambatane na matendo mema. Mambo hayo mawili kwa pamoja ni muhimu kwa ajili ya kuingia Peponi. Kwa mujibu wa Hadithi, imani, Uislamu na ihsani huunda pande tatu za dini ya Kiislamu.

Kuna midahalo ndani na nje ya Uislamu juu ya uhusiano kati ya imani na hali ya kujiridhisha kiimani katika dini, na juu ya tofauti ya umuhimu kati ya mambo hayo mawili. Baadhi ya wanazuoni wanapinga hoja ya kuwa imani na utashi wa kutaka kujiridhisha kabla ya kuamini, ni mambo mawili yatokanayo na chanzo kimoja na hutangamana. [3] [ <span title="This citation requires a reference to the specific page or range of pages in which the material appears. (February 2022)">ukurasa<span typeof="mw:Entity"> </span>inahitajika</span> ]

Etimolojia hariri

Kwa Kiarabu, imani maana yake ni hali ya kukubali na kutotilia shaka mafundisho na mtindo wa maisha ya kidini. Ni kuitambua dini kwa dhati.

Fasili na maana hariri

Katika hadithi, nabii wa Kiislamu Muhammad alifasili imani kama "kukiri moyoni, kutamka kwa ulimi, na kushughulika kwa maungo ya mwili." Imani ni kuukubali ukweli halisi pasi na mashaka. Watu wakiwa hawana wasiwasi juu ya ukweli wa jambo, hujisalimisha wenyewe mbele za ukweli huo. Kuujua tu ukweli haitoshi, bali utambuzi huo wa moyoni unapaswa kudhihirishwa kwa matamshi ya maneno yatakayoonesha kukubali kwa kwa akili timamu, shughuli zote zitazoambatana na imani hiyo. [4]

Hamiduddin Farahi, alipokuwa akielezea maana ya imani katika ufafanuzi wake, aliandika:

Mzizi wa imani: Neno imani hutumika kuelezea maana tofauti tofauti. Mojawapo ya minyumbulisho yake ya kimaana ni muumini, moja ya majina ya kihadhi ya Allah, kwa kuwa Yeye huwapa amani wale wanaomuelekea ili awape hifadhi. Neno hili ni msamiati wa wa tangia dahari na dahari wa kidini . Hivyo hiyo hakika iliyochanganyika na unyenyekevu, kutokuwa na shaka pamoja na kufuata masharti yaliyopo ya mwelekeo husika, ndiyo imani na Yule anayeelekeza imani hiyo ndiye Allah, kwa ishara zake, na kwa maelekezo yake, na anajisalimisha kwake na hufurahishwa na maamuzi yake yote, huyo ndiye muumini.

Fasili ya imani kwa mujibu wa Ahlul-Sunnah wa'l-Jama'ah ni:

Kufanya utambuzi kutokea moyoni, kutamka kwa maneno , na kutenda kupitia maungo ya mwili ; huimarishwa na utii na hudhoofishwa na dhambi .[5]

  • Ibn Abd al-Barr alisema: Kigezo:Pb
  • Al-Shafi'iy alisema katika Kitabu cha al-Umm : Kigezo:Pb
  • Muhammad bin Ismail bin Muhammad bin Al-Fadl Al-Taymi Al-Asbhani alisema: Kigezo:Pb
  • Sufyan bin ́Uyaynah alisema: Kigezo:Pb[Wote hao wamesema sasa kuwa] Watu wa haki na WA Hadithi husema kwa kauli moja kuwa imani ni khutuba na matendo, na hakuna matendo yaso dhamira.
  • ema: Kigezo:PbAl-Shafi'i alisema katika Kitabu cha al-Umm:. Na muafaka ukapatikana kutoka kwa masahaba wa kadhalika Tabi'een. Baada ya kipindi chao ndipo tulipofahamu kwamba imani ni maneno pamoja na matendo, na dhamira ni mojawapo ya utatu huo, bila mojawapo mengine hayatoshi.
  • Muhammad bin Isamail bin Muhammad bin Al-Fadl Al-Taymi Al-Asbhani alisema: "Na imani katika lugha ya sharia ni kutia saini na kupitisha jambo kutoka moyoni kisha kufanya matendo kupitia maungo".
  • Sufiani Ibn Uyaynah alisema:
  • " Imani ni kusema kutenda, huongezeka na hupungua."
  • Al-Ash'ari said: "Kwa kauli moja wamekubali kuwa imani (hali ya kukiri na kukubali moyoni) huimarika kupitia utii na hudhoofika kupitia dhambi, na utovu wake haumaanishi kuwa tuna mashaka juu ya yale tunayoamrishwa kuyaamini, wala kukosa kwetu kujua, Kwa sababu hiyo ni kufuru au kukataliwa kutoka kwenye mkondo wa kidini, badala yake itakuwa ni kuporomoka kutoka kwenye ngazi za ujuzi au kimawazo na ni kuimarika kwenye upande wa mithali zetu, kama ilivyo hivyo, uzani wa utii wetu na utii wa Mtume Muhammad (s.a.w) vyatofautiana, hata kama wote tunatekeleza majukumu yetu.

Misingi Sita ya Imani hariri

Kuna misingi sita ya imani:

1. Kuamini kuwa Mungu yupo na hana mshirika.

2. Kuamini juu ya uwepo wa malaika.

3. Kuamini juu ya uwepo wa vitabu vilivyoandikwa na Mungu:

Kuruani (aliyoshushiwa Muhammad, s.a.w)

Injili (aliyokabidhiwa Mtume Issa)

Torati (waliyokabidhiwa mitume)



Zaburi (aliyokabidhiwa Daudi)

Majuzuu ya Musa






Majuzuu ya Abrahamu

4. Kuamini juu ya uwepo wa Mitume: Muhammad akiwa ndiye Mtume wa mwisho, Mtume Issa akiwa ni WA pili kutoka mwisho, na wengine waliokuwepo kabla yao (kama Musa, Abrahamu, Daudi, Yusufu na Yakubu)

5. Kuamini juu ya uwepo Siku ya Kiyama: kwenye siku hiyo binadamu watagawanywa katika makundi mawili: lile la Peponi na lile la Jehanamu. Makundi hayo yatakuwa yakifanywa na makundi mengine madogo.

6. Kuamini yakuwa Mungu ndiye mpangaji wa yote (muweza wa yote na anajua yote, hata yajayo), mabaya na mazuri.

  1. he Torah (revealed
  2. groups are composed of subgroups.
  3. predestinationKigezo:Transliteration, Kigezo:Gloss

Kati ya hii, minne ya kwanza imetajwa na wa tano umemaanishwa katika ayah 2:285 ya Kuruani. Yote sita inaonekana katika hadith ya kwanza ya mkusanyiko wa maandiko ya Sahih Muslim, ambapo malaika Jibril anauliza kuambiwa juu ya iman na Muhammad anajibu:Unadhihirisha Kwa uthabiti imani yako kwa Allah, kwa malaika wake, katika Vitabu vyake, kwa Mitume wake, juu ya Siku ya Kiyama, navunadhihirisha imani yako juu ya Uweza wa kipekee wa Mungu juu ya mazuri na mabaya.

Maelezo mengine yanayofanana na hayo yanayohusishwa na Muhammad ni:Ibn Abbas anaeleza kuwa malaika Jibril alipata kujiuliza Mtume: "Niambie, Uislamu ni nini?"

Mtume akamjibu: "Imani ni kuamini juu ya uwepo wa Allah, Siku ya Kiyama, Malaika wake (Allan), Vitabu na Mitume na kuamini juu ya maisha baada ya kifo; na kuamini juu ya Peponi na Moto wa Jehanamu, na kufanyika kwa hukumu kupitia Mizani ya kupimia amali za watu; na kuamini juu ya Uweza wa Allah usio na mipaka na uzur na ubaya wake.

Kisha Jibril akamuuliza: " Nikifanya yote hayo, nitakuwa na imani?"

Mtume akamwambia: "Utakapofanya yote hayo, utakuwa mwenye imani"

Ufafanuzi katika Qur'an na Hadith hariri

 
Pande tatu za Uislamu ikiwemo imani .

Katika Kuruani, imani ni miongoni mwa sifa 10 zinazomfanya mtu kuwa mpokeaji wa rehema na thawabu za Mwenyezi Mungu. Qur'an inasema kwamba imani inaweza kukua kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Qur’ani pia inasema kuwa hakuna kitu katika dunia hii kinachopaswa kupendwa zaidi na Muumini wa kweli kuliko imani.

Muhammad anaripotiwa kusema kwamba alionja utamu wa imani na alikuwa radhi kumkubali Mungu kama Bwana, Uislamu kawa dini na Muhammad ndiye Mtume wake [6] Vile vile alisema kuwa hakuna anayeweza kuwa muumini wa kweli bali kwa kumpenda Muhammad zaidi ya anavyowapenda watoto wake, wazazi na jamaa zake. [7] [8] Katika tukio jingine, alisema kwamba ni upendo wa namna hii kwa Allah na Muhammad utaomfanya mtu aweze kuitambua ladha halisi ya imani. [9] [10]

Amin Ahsan Islahi, mfafanuzi mashuhuri wa Kuruani amefafanua asili ya upendo huu:

Haimaanishi tu ule upendo wa huba ambao kwa asili mtu anao kwa mkewe, watoto na ndugu wengine, lakini hurejea pia juu ya upendo unaotokana na hekima na kanuni za masula na mambo maalum. Ni Kwa sababu ya upendo huu ambapo mtu, katika nyanja zote za maisha, anaweka kipaumbele kwenye mtazamo na mwelekeo huu. ... Hivyo ndivyo ilivyo, kama matakwa ya mkewe, watoto na nduguze yatapingana na matakwa ya mtazamo huu, atabaki mnyoofu kwenye mtazamo wa imani na bila kusita atayabwaga matamanio ya mkewe, na ya wanawe na matakwa ya jamaa zake na ukoo.[11]

Islahi na Abul A'la Maududi wote wamedokeza kwamba ulinganisho wa Kuruani wa neno zuri na neno baya katika sura ya 14 ni ulinganisho wa imani na ukafiri. Hivyo, Kuruani inalinganisha kwa ufanisi suala la imani na mti ambao mizizi yake iko ndani kabisa ya udongo na matawi yaliyotandaa kama mbingu. [12]

Pia Imani ni kitovu cha maombi ya unyenyekevu ya Muhammad aliyomwambia Mungu:

Ewe Mola wangu! Nimejitoa kwako na nimeliweka jambo langu mbele zako na nimepata msaada toka kwako nikihofia ukuu wako na kujongea karibu yako kwa matumaini. Hakuna kimbilio na hifadhi kama nitakukimbia, na kama kuna kimbilio basi ni kwako. Bwana! Nimelitangaza Neno lililo kwenye Kitabu chako, ulilonishushia, ambalo nalo limemtangaza Mtume wako uliyemtuma kuwa mjumbe wako.[13]

Matawi Sabini na Saba ya Imani hariri

"Matawi Sabini na Saba ya Imani" ni mkusanyiko uliokusanywa na imam Shafi'i al-Bayhaqi katika kazi yake iitwayo Shu'ab al-Iman . Kwenye kazi hiyo, anaeleza maadili muhimu yanayoakisi iman ya kweli (imani na utambuzi) kupitia aya za Kuruani zinazohu maneno ya manabii. [14] [15]

Hili linatokana na Hadithi ifuatayo ya Mtume Muhammad:

Abu Hurayrah alieleza kuwa Mtume alisema: "Imani Ina zaidi ya matawi 70. Lililo zuri kuliko yote kati ya hayo ni msemo "Laa ilaaha I'll Allah" (Hakuna Mungu wa haki ila Allah) na tawi dogo kuliko yote ni tendon la kuondoa kikwazo kutoka njiani. Pia, "Haya" ni tawi muhimu la imani.Matawi 77 yaliyoelezwa na Bayhaqi ni: [16]

Vitendo thelathini vinavyoongozwa na moyo:

  1. Imani Katika Mwenyezi Mungu (Ushuhuda wa kukiri: La ilaha illallah' (hakuna mungu wa kweli isipokuwa Mwenyezi mungu)
  2. Kukubali kwamba hapo mwanzo hakukuwa na chochote bali Mwnyezi Mungu naye ndiye aliyeumba kila kitu.
  3. Kutambua kuwepo kwa malaika (malaikah).
  4. Kukiri kwamba vitabu vyote vitakatifu (qutub) kutumwa kwa Manabii mbalimbali ni kweli. Hata hivyo, vitabu vyote isipokuwa Qur'ani havifai tena.
  5. Kutambua kwamba manabii wote ni wa kweli. Hata Hivyo, Waislamu wanaamriwa kufuata tu nabii Wa Kiislamu, Muhammad
  6. Kuamini Kwamba Mwenyezi mungu tayari anajua kila kitu na kwamba chochote anachoruhusu au anachotaka kitatokea.
  7. Kuamini Kwamba Siku ya Mwisho itatokea.
  8. Kutambua kuwepo kwa Jannat (Paradiso).
  9. Kutambua kuwepo Kwa Jahannamu
  10. Kuwa na upendo Kwa Mwenyezi mungu.
  11. Kutambua upendo Wa Muhammad Kwa Allah
  12. Kumpenda au kumchukia Mtu kwa Ajili Ya Mwenyezi mungu tu.
  13. Kufanya matendo mema yote kwa uaminifu (kusudi la deen ila kumridhisha Mwenyezi mungu.
  14. Kutubu na kuonyesha majuto wakati dhambi imefanywa.
  15. Mcheni Mwenyezi mungu.
  16. Tumaini la rehema ya Mungu.
  17. Kuwa mnyenyekevu.
  18. Kuonyesha shukrani (shukr) kwa ajili ya neema au neema.
  19. Kutimiza ahadi.
  20. Kuwa na subira (sabar).
  21. Kujisikia duni kwa wengine.
  22. Kuwa mwema kwa uumbaji wa Mungu. [<span title="The text near this tag may need clarification or removal of jargon. (February 2023)">ufafanuzi unahitajika</span>]
  23. Kuridhika na maagizo yoyote yaliyoamriwa hutoka Kwa Mwenyezi Mungu
  24. Kumtegemea Mwenyezi mungu.
  25. Sio kujivunia au kujisifu juu ya ubora wowote ambao mtu anao
  26. Sio kumchukia au kumchukia mtu yeyote.
  27. Usiwe na wivu kwa mtu yeyote.
  28. Sio kukasirika.
  29. Sio kumtakia mtu yeyote madhara.
  30. Kutokuwa na upendo kwa ulimwengu.

Kazi saba zinazothibitisha maneno hayo:

  1. Kutamka Kalima kwa maneno.
  2. Kusoma Quran.
  3. Kutafuta elimu.
  4. Kutoa maarifa
  5. Kuomba dua .
  6. Zikiri kwa Mwenyezi Mungu.
  7. Kujiepusha na mambo yafuatayo: kusema uwongo, kusengenya (kukashifu mtu wakati hayupo), mambo machafu, yalolaaniwa, na kuimba nyimbo za matusi zinazopingana na Sharia.

Kazi arobaini zinazothibitisha mafundisho yote :


  1. Kutawadha, kuoga na kuweka mavazi katika hali ya usafi.
  2. Kutotetereka juu ya swala.
  3. Kutoa zaka na sadaka Kigezo:Transliteration and Kigezo:Transliteration
  4. Kufunga Ramadhani
  5. Kwenda hija Kigezo:Transliteration.
  6. Kufanya itikafu Kigezo:Transliteration.
  7. Kujitenga na au kuhama kutoka, neneo lenye husda dhidi ya dini.
  8. Kutekeleza nadhiri uliyoiweka kwa Allah.Kigezo:Which[<span title="The material near this tag possibly uses too vague attribution or weasel words. (February 2023)">which?</span>]
  9. Kutekeleza viapo visivyokuwa vya dhambi.
  10. Kulipa sadaka maalum kwa ajili ya yale aliyoshindwa kutekeleza.
  11. Kuuhifadhi vema mwili kwa mavazi.
  12. Kujitoa mhanga kwa ajili ya Allah.
  13. Kuizika maiti kwa kuivika sanda.
  14. Kulipa madeni.
  15. .
  16. Kutovunja miiko iliyowekwa wakati wa kufanya miamala ya kifedha.
  17. Kutoficha ukweli wakati wa kutoa ushuhuda.
  18. Oa wakati nafsi inakutaka uoe.Kigezo:Transliteration
  19. Kuwaruhusu walio chini yako watekeleze yaliya ya haki kwao.
  20. Kuwafariji wazazi.
  21. Kuwakuza watoto katika malezi mema.
  22. Kutovunja uhusiano na ndugu au marafiki.
  23. Kuwatii wakubwa wa kazi.
  24. Kuwa mtu wa haki na mwongofu.
  25. Kutoasi Uislamu na misingi yake.
  26. Kumtii mtawala, kama ayaamrishayo hayaendi kinyume na sharia.
  27. Kuzisuluhisha pande mbili zinazopigana vita au wawili wagombanao.
  28. Kutoa msaada kwa vuguvugu lenye manufaa. .Kigezo:Which[<span title="The material near this tag possibly uses too vague attribution or weasel words. (February 2023)">which?</span>]
  29. Kulingania mema na kukataza mabaya. (Kigezo:Transliteration).
  30. Kama ni serikali, basi itoe adhabu kwa mujibu wa sharia.[clarification needed][<span title="What does this sentence mean? What is 'it'? (February 2023)">clarification needed</span>]
  31. Kupambana dhidi ya maadui wa dini (ikiwezekana kwa mapigano , kama si kwa maneno (Kwa kalamu), kama si moyoni ).
  32. Kulipa amana za ahadi au nadhiri. [<span title="Which deposit? Deposits in general? (February 2023)">clarification needed</span>]
  33. Kuwakopesha wenye uhitaji.
  34. Kuwasaidia jirani wenye shida.
  35. Kuhakikisha kipato ni cha halali na kutakasika.
  36. Matumizi yaongozwe na Shariah.
  37. Kumwitikia anayekusalimu.
  38. Kigezo:Transliteration Kujibu yarhamukallah kwa aliyepiga chafya na kusema alhamdulillah. Kigezo:Transliteration after sneezing.
  39. Usimuumize yeyote Kwa kumwonea.
  40. Kujizuia dhidi ya michezo na mambo mengine yapotezayo muda na yalo kinyume cha sheria.
  41. Kuondoa kokoto, mawe, miba, matawi, nk. kutoka barabarani.

Imani na matendo hariri

Katika Uislamu, lazima kuwe na utangamano na kukubalina vilivyo kati ya imani na matendo. Farahi amekieleza kipengele hiki katika tafsiri yake kwa namna ifuatayo: [17]

Matendo yaliyoongoka yametajwa katika Kuruani mara baada ya suala la imani kwa nguvu za hoja [...] Kwa upande wa imani, haja ya kuielezea ni dhahiri: nafasi ya imani ni ya moyoni na ya hekima. Katika Masuala yahusuyo hekima na ya moyoni, sio tu mtu anaweza kudanganya wengine, lakine nyakati nyingine, anaweza kubaki akijidanganya. Anajiona yeye ni muumini wakati ukweli ni kuwa, sio. Kwa sababu hii , shuhuda mbili zahitajika juu ya hilo: maneno ya mtu na matendo yake. Kwa kuwa maneno yaweza kuwa ya uongo, hivyo mtu atangazae imani kwa maneno hachukuliwi kuwa muumini na ikaamuliwa kuwa ni muhimu matendo yake pia yatoe ushuhuda juu ya imani yake.

Imani na hali ya kujiridhisha kiimani katika Uislamu hariri

Uhusiano kati ya hali ya kujiridhisha kabla ya kuamini na imani katika Uislamu ni mdahalo mgumu uliodumu karne nyingi. Ismail Raji al-Faruqi anatamka kuhusu suala hili:

Kwa wale wasio Waislamu, wanaweza wakapingana na kanuni za Uislamu . Lakini yawapasa wajue kuwa Uislamu hauwasilishi kanuni zake kimabavu na pasipo kuhojiwa, kwa waamini na wale waelekeao kuamini tena kwa kuwatenganisha. Hufanya hivyo kwa njia inayokubalika na inayoruhusu utunduizi. Kanuni huwasilishwa kwetu Kwa hoja zenye mantiki na mashiko, na hutarajia kukubali kwetu katika mazingira huru ya msingi. Ni kinyume cha sheria kwetu kutokubali dhana ya uchaguzi ya wale walinganishi wa mambo au mawazo na hisia binafsi za wengine.of personal taste, or that of subjective experience.[18]

[[Jamii:Imani]] [[Jamii:Dini ya Kiislamu]] [[Jamii:Pages with unreviewed translations]]

  1. Farāhī, Majmū'ah Tafāsīr, 2nd ed. (Faran Foundation, 1998), 347.
  2. Frederick M. Denny, An Introduction to Islam, 3rd ed., hp. 405
  3. Islahi, Amin Ahsan. Mabadi Tadabbur-i-Hadith (translated: Fundamentals of Hadith Interpretation)
  4. Murata & Chittick 1994.
  5. "الموسوعة العقدية". dorar.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Muslim, Al-Jami' al-sahih, 38, (no. 151).
  7. Al-Bukhari, Al-Jami' al-sahih, 6, (no. 15)
  8. Muslim, Al-Jami' al-sahih, 41, (no. 169)
  9. Al-Bukhari, Al-Jami' al-sahih, 6–7, (nos. 16, 21)
  10. Muslim, Al-Jami' al-sahih, 40, (no. 165)
  11. Amin Ahsan Islahi, Tazkiyah-i nafs (translation: Self Purification), 119
  12. Amin Ahsan Islahi, Tazkiyah-i nafs, 325.
  13. Al-Bukhari, Al-Jami' al-sahih, 45, (no. 247)
  14. "The 77 Branches of Faith - Shafii". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-10. Iliwekwa mnamo 2006-07-09.
  15. "Central-Mosque.com redirector to the new design". www.central-mosque.com. Iliwekwa mnamo 15 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "77 Branches of Faith". Islam.org.uk (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 15 Aprili 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. Farāhī, Majmū'ah Tafāsīr, 2nd ed.
  18. Isma'il Raji al Faruqi, Islam and Other Religions