Mtumiaji:Rwebogora/Yuyun Ismawati

Yuyun Ismawati (alizaliwa 1964) ni mhandisi wa mazingira kutoka Indonesia. Amefanya kazi katika kubuni mifumo ya usambazaji maji mijini na vijijini, na baadaye kubuni mifumo ya usimamizi wa taka salama. Alitunukiwa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mnamo 2009.[1]

Ni Mshauri Mkuu na mwanzilishi mwenza wa BALIFOKUS Foundation, Shirika Lisilo la Kiserikali la mazingira lenye makao yake makuu Bali. Yuyun ana uzoefu mpana na tajiri katika masuala ya usimamizi wa mazingira mijini, afya ya mazingira na usafi wa mazingira, pamoja na masuala ya hali ya hewa na sumu.[2]

Marejeo hariri

  1. "Yuyun Ismawati". Goldman Environmental Prize. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Yuyun Ismawati". Project Southeast Asia (kwa American English). 2012-12-22. Iliwekwa mnamo 2016-05-27.