Musa Bilankuli

mwanasoka

Musa Bilankulu (alizaliwa 22 Februari 1985, Vosloorus) ni mwanasoka wa kulipwa nchini Afrika Kusini ambaye mara ya mwisho aliichezea katika timu ya Bizana Pondo Chiefs, kama beki.

Maisha ya Soka hariri

Bilankulu alianza kazi yake kwenye klabu ya Golden Arrows mwaka 2005. Baadaye alichezea katika timu ya Bidvest Wits, Bloemfontein Celtic, Golden Arrows na Bizana Pondo Chiefs. Alisajiliwa na timu ya Bizana Pondo Chiefs mnamo Desemba 2020, kwa mkataba hadi mwisho wa msimu.

Soka kimataifa hariri

Alipokea wito wake wa kwanza kuichezea timu yake ya taifa ya Afrika Kusini mnamo Novemba 2011. Bilankulu alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu mnamo Machi 2020.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Musa Bilankuli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.