"My Life" ni kibao cha tatu cha rapa The Game kutoka katika albamu yake ya tatu, LAX ambao ilitolewa mnamo tar. 22 Agosti 2008. Wimbo umetayarishwa na Cool na Dre, ukimshirikisha Lil Wayne, na ipo kama jinsi nyimbo zake nyingi za karibuni alizotoa Lil Wayne, anatumia kionjo cha Auto-Tune kwa ajili ya kiitikio.

“My Life”
“My Life” cover
Single ya The Game akimshirikisha Lil Wayne
kutoka katika albamu ya LAX
Imetolewa 22 Julai 2008 (U.S.)
5 Agosti 2008 (iTunes)
Muundo CD single
Digital Download
Imerekodiwa 2008
Aina West Coast hip hop, Hip hop
Urefu 5:27 (album version)[1]
4:35 (extended radio edit)[1]
3:38 (main radio edit)[1]
Studio Geffen/Interscope
Mtunzi Jayceon Taylor
Dwayne Carter, Jr.
Mtayarishaji Cool na Dre
Mwenendo wa single za The Game akimshirikisha Lil Wayne
"Dope Boys"
(2008)
"My Life"
(2008)
"House of Pain"
(2008)


na tarehe zake
"Can't Believe It"
(2008)
{{{Albamu}}} "Let It Rock"
(2008)

Historia hariri

Kurekodi hariri

Watayarishaji Cool na Dre wametoa makala ya video yanayoonyesha namna walivyotengeneza biti la wimbo huu.[2]

The Game alizungumza juu ya kazi yake waliyofanya na Lil Wayne na kueleza:

Unapokuwa ndani ya studio na Wayne, unaweza kutulia sana yaani, mshikaji, kwa sababu kila kitu kina kuwa rahisi kinoma. Anaweza kwenda na mamelodi ajabu. Pindi apigapo na ma-idea, au niibuke na ma-idea, tunanyoosha, mwana. Mchakato wake ni rahisi. Ninafikiri mimi na yeye labda tungeweza kufanya albamu, kama, sikui saba hivi. Albamu bab-kubwa! Anaiwekea 100, naiwekea 100. Sote ni Ma-MC wenye vipaji. Nakumbali sana kwenye hip-hop.[3]

Nafasi ya chati hariri

"My Life" ilitolewa kwa mara ya kwanza kupiti maduka ya iTunes huko Amerika ya Kaskazini kwa ajili upakuaji wa dijitali. Nchini Marekani, iliingia kwa kushika nafasi ya #21 kwenye chati za Billboard Hot 100 inaifanya kuwa kibao pekee cha The Game kushika nafasi ya juu sana kwenye chati. Pia iliingia na kushika nafasi ya #32 kwenye Pop 100 ambayo pia inashughulika na masuala ya upakuaji mkondoni. Huko nchini Kanada iliingia na kushika nafasi ya #42 kwenye chati za Canadian Hot 100 na wiki hiyohiyo pia ikaingizwa kwenye orodha upakuaji mkondoni. Kwenye chati za UK Singles Chart ma kushika nafasi ya #34.

Chati (2008) Nafasi
iliyoshika
Canadian Hot 100[4] 42
U.S. Billboard Hot 100[5] 21
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs 15
U.S. Billboard Hot Rap Tracks 4
U.S. Billboard Mainstream R&B/Hip-Hop 9
U.S. Billboard Pop 100 32
Irish Singles Chart 32
Swiss Singles Chart 49
UK Singles Chart[6] 34

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 According to single cover.
  2. 305 Uncut Presents Making The Beat Cool & Dre "My Life" Part 1 Archived 12 Septemba 2008 at the Wayback Machine. Accessed 23 Agosti 2008.
  3. Andres Tardio (18 Agosti 2008) Why Did Game Say "Hip Hop Broke My Heart?" Archived 5 Januari 2009 at the Wayback Machine. HipHopDX. Accessed 21 Agosti 2008.
  4. Billboard Canadian Hot 100. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-12-21. Iliwekwa mnamo 2009-12-29.
  5. Billboard.com - Artist Chart History - The Game. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-08-22. Iliwekwa mnamo 2008-08-22.
  6. The Official UK Charts Company: TOP 100 SINGLES CHART