Nakaaya

Mwimbaji na mwimbaji wa rap wa Tanzania.

Nakaaya Abraham Sumari (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Nakaaya tu; amezaliwa 3 Septemba 1982, Arusha mkoa wa Kaskazini mwa Tanzania) ni mwimbaji wa muziki wa R&B, Hip hop, na dansi kutoka nchini Tanzania.

Nakaaya
Nakaaya akiwa katika pozi
Nakaaya akiwa katika pozi
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Nakaaya Abraham Sumari
Amezaliwa 3 Septemba 1982 (1982-09-03) (umri 41)
Asili yake Arusha, Tanzania
Aina ya muziki R&B, Hip hop, dansi
Kazi yake Rapa
Ala Sauti
Miaka ya kazi 2004 - hadi leo
Studio 41 Records
Tovuti Tovuti ya Nakaaya

Anajulikana sana kwa kibao chake mashuhuri cha Mr. Politician. Huyu ni dada ya aliyekuwa mrembo wa Tanzania kwa mwaka wa 2005, Nancy Sumari.

Wasifu hariri

Maisha ya awali hariri

Yeye ni wa kwanza kuzaliwa kutoka katika familia ya watoto watano. Wazazi wake ni wafanyabiashara huko mkoani Arusha. Nakaaya alikulia mjini Arusha na Nairobi, Kenya, ambapo alikwenda kwa sababu za kimasomo. Akiwa bado yungali mdogo, Nakaaya alipenda sana kuimba na kutumbuiza.

Baada ya kumaliza shule, alihamia jijini Dar es Salaam na akawa anafanya kazi katika nyanja kadhaa za kitawala kabla hajajiendeleza na masuala ya kimuziki. Nakaaya alishawahi kufanya kazi na bendi ya Tanzanite ambao walimwalika ili wafanyenaye kazi kunako mwaka wa 2004. Lakini, ilimlazimu kusimamisha shughuli za muziki kwa muda ili isije ikaingliana na kazi zake za kila siku.

Mnamo mwaka wa 2006, akapata nafasi katika moja kati ya matamasha ya Tusker Project Fame ambayo yalifanyika katika jumba la Dar Cinemas. Nakaaya akapata bahati ya kumvutia mmoja wa wa majaji kwa uwezo wake na kipaji alichonacho. Hivyo akawa mmoja kati ya waamuru katika kipindi hicho.

Viungo vya Nje hariri

  • Nakaaya katika Tanzania Directoty.info
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nakaaya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.