Nancy Kalembe

Mwanasiasa wa Uganda


Nancy Linda Kalembe (alizaliwa mnamo mwaka 1980) ni mwanasiasa kutokea nchini Uganda.

Nancy Kalembe
Alizaliwa 1980
Nchi Uganda
Kazi yake Mwanasiasa
Wazazi George Patrick Bageya na Cissy Kubaaza
Watoto 2

Aligombea urais mnamo mwaka 2021, ambapo alikuwa mwanamke pekee kugombea, ila alishindwa na mpinzani wake Yoweri Museveni.

Maisha ya Awali naElimu hariri

Nancy Kalembe alizaliwa mwaka 1980 na kukulia katika wilaya ya Iganga nchini Uganda katika mkoa wa Busoga.[1][2][3] Alikuwa ni mmoja wa watoto kumi na nane katika familia yao na baba yake alikuwa akiitwa George Patrick Bageya aliekuwa mwanasiasa na mama yake aliitwa Cissy Kubaaza aliefariki wakati Nancy akiwa na umri wa miaka kumi na tatu.[2][3][4]

Kalembe alihitimu katika chuo kikuu cha Makerere mwaka 2017.

Maisha binafsi hariri

Kalembe aliolewa mwaka 2007, lakini baadae alikuja kutalikiana na mume wake, na katika kipindi cha ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili.

Marejeo hariri

  1. Athumani, Halima (2021-01-11). "Uganda's Only Female Presidential Candidate Says Leadership Needs to Change". Voice of America (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-04.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  2. 2.0 2.1 Oluka, Esther (2020-11-14). "I will not be intimidated out of the presidential race- Nancy Kalembe". Daily Monitor (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-05.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  3. 3.0 3.1 "Nancy Kalembe, Could She Become Ugandas First Woman President?". Uganda Radio Network (kwa Kiingereza). 2021-01-13. Iliwekwa mnamo 2021-02-05.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  4. Ahabwe, Conrad (2020-07-05). "Who is Nancy Kalembe, the female presidential aspirant?". PML Daily (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-02-05.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nancy Kalembe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.