Nassim Akrour (alizaliwa 10 Julai 1974) ni mwanasoka na kocha wa klabu za Kifaransa na Algeria ambaye kwa sasa yuko klabu ya Chambéry na kufundisha timu ya vijana ya Annecy, ambaye aliwakilisha kama mchezaji kati ya mwaka 2016 na 2019. Katika ngazi ya kimataifa Nassim ameiwakilisha Algeria, Kwa kucheza mechi 18 na kufunga mabao sita kati ya mwaka 2001 na 2004.

Ain Sud Foot - Chambéry Savoie Football (2020-09-12) - Nassim Akrour.jpg

Ushiriki Katika Kllabu hariri

Akrour alizaliwa huko Courbevoie, Ufaransa. Alianza uchezaji wake katika klabu ya Olympique Noisy-le-Sec,Akrour alihamia Uingereza mwaka 1997 ili kujiunga na klabu ya Sutton United, ambapo alifunga mabao 19 katika mechi 41 katika msimu wa 1998-99. [1]

Ushiriki Kimataifa hariri

Mnamo 5 Desemba 2001, Akrour aliichezea timu ya taifa ya Algeria kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 60 katika mechi ya kirafiki na Ghana mjini Algie. Pia alikuwa sehemu ya timu ya Algeria ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2004, ambayo ilimaliza ya pili katika kundi lao katika mzunguko wa kwanza wa mashindano kabla ya kushindwa na Morocco katika robo-fainali.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nassim Akrour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.