Nazareti (الناصرة kwa Kiarabu, נצרת kwa Kiebrania) ni mji wenye watu 77,445[1] upande wa kaskazini wa nchi ya Israeli, ambao kihistoria unajulikana kama Galilaya.

Kisima cha Bikira Maria - Kisima cha karne ya 1 ni kielelezo cha mji wa Nazareti.

Wakazi wengi ni raia wa Israeli wanaoongea Kiarabu na kufuata dini za Uislamu (68,7%) na Ukristo (31,3%).

Nazareti unajulikana kama mji walipokulia Bikira Maria na mwanae Yesu Kristo, ambaye kadiri ya Injili, ingawa alizaliwa Bethlehemu, alikuwa anatajwa kama Mnazareti.

Marejeo hariri

  1. "Population in the Localities 2019" (XLS). Israel Central Bureau of Statistics. Retrieved 16 August 2020.

Viungo vya nje hariri