Neoni (kutoka Kigiriki νέος neos - "mpya") ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 10 na uzani wa atomi 20.1797. Alama yake ni Ne.

Neoni (Neon)
Herufi za Ne zang'aa kwa sababu zinaonyeshwa kwa tubu zinazojaa Neoni
Herufi za Ne zang'aa kwa sababu zinaonyeshwa kwa tubu zinazojaa Neoni
Jina la Elementi Neoni (Neon)
Alama Ne
Namba atomia 10
Mfululizo safu Gesi adimu
Uzani atomia 20.1797
Densiti 0.9002 g/L
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 24.56 K (-248.59 °C)
Kiwango cha kuchemka 27.07 K (-246.08 °C)
Asilimia za ganda la dunia 5 · 10-7  %
Hali maada gesi

Duniani yapatikana katika angahewa kama gesi adimu na bwete isiyo na rangi wala ladha. Kwa sababu ya tabia yake ya ubwete kampaundi zake hazijulikani.

Lakini pia Neoni ni elementi iliyo imara na isiyochanganyikana kikemikali na elementi nyingine katika hali ya kawaida.

Neoni yapatikana kwa wingi katika anga la ulimwengu lakini ni haba duniani. Ni gesi adimu, nyepesi zaidi duniani baada ya heli.

Matumizi hariri

Neoni ikipitishwa na umeme yatoa mwanga mwekundu, hivyo yatumiwa katika taa memetevu na matangazo memetevu.

Inatumiwa pia katika teknolojia ya friji kama kizizimshi.

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.