'

Njenga Karume
Njenga Karume
Amezaliwa1929
Kazi yakeMfanya biashara wa kenya


James Njenga Karume (alizaliwa mnamo mwaka wa 1929) ni mwanasiasa mkongwe wa Kenya.

Biashara hariri

Karume ana diploma katika Usimamizi wa Biashara kutoka Jeans School (KIA). Wakati Kenya ilikuwa bado chini ya utawala wa kikoloni, alianzisha duka katika barabara ya Grogan (sasa barabara ya Kirinyaga) mjini Nairobi. Ilikuwa moja kati ya maduka chache nchini Kenya kuendeshwa na watu asili ya Kikenya.

Baadaye aliendesha kampuni ya Nararashi Distributors, ambayo walikuwa na wadhifa wa kusambaza bidhaa za Kenya Breweries Limited (KBL). Baadaye Castle Brewing Kenya Limited, kampuni ndogo(subsidiary) nchini Kenya ambacho kampuni yake kuu ni South African Breweries (SAB) iliundwa, huku Karume akiteuliwa kama mkurugenzi wake. Karume mwenyewe alitaka kusambaza bidhaa za kampuni zote mbili, lakini KBL iliofia ushindani na kuamua kufutilia mbali mkataba wa Karume wa usambazaji ili kudhuru biashara yake. Karume alichukua kesi mahakamani na kusema kuwa kufutilia mbali kwa mkataba wake haukuwa na ushahidi. Mahakama Kuu kwanza iliamuru KBL kumlipa Karume Shilingi za Kenya 231 kwa uharibifu lakini kutokana na rufaa uamuzi ulipinduliwa na Karume aliambiwa kulipa KBL kwa mashtaka. Kutokana na malipo hayo kwa KBL, Karume aliathiriwa na uhaba wa fedha. Aliendelea kusambaza bia ya Castle kwa muda hadi SAB ilipoondoka Kenya, hatimaye kukamilisha biashara yake ya usafiri.

Siasa hariri

Karume alikuwa mwanasiasa biabia katika shirika la G.E.M.A ambalo lilikuwa chama cha kisiasa. Wakati Jomo Kenyatta bado alikuwa rais wa Kenya, mwaka wa 1976, Karume alijiunga na idadi ya wanasiasa wengine wakijumuisha Kihika Kimani na Paul Ngei na kuunda harakati ya "Change the Constitution Movement" kujaribu kubadilisha Katiba ya Kenya kama kwamba Makamu wa rais wa wakati huo Daniel arap Moi asingeweza kurithi urais kutokana na kifo cha Kenyatta. Harakati hii kwa ufupi ilitaka kumzuia rais asiye wa jamii ya Wakikuyu. Harakati hii haikudumu kwa muda mrefu. Mwanasheria Mkuu Charles Njonjo, mwenyewe pia na ndoto za urais, aliwashtaki Karume na viongozi wengine wa harakati hiyo na uhaini, kwani "walikuwa wamefikiria kifo cha rais ambaye bado alikuwa hai", dhana ambayo ilikuwa imekatazwa na sheria. Rais Kenyatta alishukisha mashtaka, lakini wakati huo huo aliinyamazisha harakati.

Kati ya mwaka wa 1979 alihudumu kama mbunge wa kuteuliwa Mwaka wa 1979 alichaguliwa kama mbunge wa eneo bunge la Kiambaa na alikuwa alichaguliwa tena miaka ya 1983 na 1988. Tangu mwaka wa 1979 alishikilia nyadifa mbalimbali za msaidizi wa mawaziri. Aliiwakilisha KANU, wakati huo hicho ndicho kilikuwa chama cha kisiasa kinachotambulika kihalali na sheria nchini Kenya.

Katika Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe katika uwanja wa Kasarani katikati ya mwaka wa 1991 Karume aliongoza msukumo wa kuikataa Sehemu 2A ya Katiba ya Kenya – ambayo ilikuwa marejesho ya mfumo wa vyama vingi. Rais Moi hakuwa na budi ili kukubali azimio.

Karume alisita kujiunga na kikosi kilichokuwa kinaongoza cha upinzani Forum for the Restauration of Democracy (FORD), kwani alikuwa amekiona chama hiki kikivunjika. Badala yake, alianzisha chama cha Democratic Party (DP) pamoja na Mwai Kibaki na John Keen mnamo 31 Desemba 1991. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 1992 Karume alisimama kwa tiketi ya DP, lakini alipoteza kiti chake kwa Kamau Icharia wa FORD-Asili, ambaye mgombea wake wa urais Kenneth Matiba alikuwa na umaarufu mkuu katika eneo bunge lake.

Alipata kiti chake cha ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 1997 na alisimama tena kwa tikiti ya DP. Katika Uchaguzi ya mwaka wa 2002 alishinda kiti hicho tena, lakini sasa kwa tiketi ya KANU huku akimunga mkono mgombea urais wao Uhuru Kenyatta, licha ya urafiki uliyosimama wa muda mrefu kati yake na mgombea urais Kibaki.

Pia alishinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002. Mnamo Desemba mwaka wa 2006, aliteuliwa kama Waziri wa Ulinzi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 aliiwakilishwa muungano wa PNU uliyokuwa unaongozwa na Rais Kibaki, lakini alipoteza kiti chake kwa Stanley Munga Githunguri wa chama cha KANU.

Mwaka wa 2009 alitoa tawasifu yake iliyokuwa inajulikana kama 'Beyond Expectations: From Charcoal to Gold'

Mkewe Njenga, Maryanne Wariara Karume aliaga dunia mwaka wa 2003.

Marejeo hariri