Katika jiografia, Oasisi ni eneo lenye mimea katikati ya jangwa, kwa kawaida likizunguka chemchemi au chanzo kingine cha maji. Oasisi pia hutoa makazi kwa wanyama na hata binadamu kama eneo ni kubwa vya kutosha.

Ein-Kelt, an Oasis in the Judean Desert, Israel

Maeneo yenye oasisi yamekuwa muhimu kwa biashara na njia za usafiri katika maeneo ya jangwa. Misafara hulazimika kupitia karibu na oasisi ili kujiongezea akiba zao za maji na chakula. Hivyo, kudhibiti kisiasa au kijeshi Oasisi mara nyingi kunamaanisha kudhibiti biashara ya misafara fulani. Kwa mfano, oasisi za Awjila, Ghadames na Kufra iliyoko katika Libya ya leo, kwa nyakati mbalimbali zimekuwa muhimu kwa biashara za Kaskazini-Kusini na Mashariki-Magharibi katika biashara ya ng'ambo ya Sahara.

Neno Oasisi liliingia katika Kiingereza kutoka neno la Kigiriki ὄασις Oasis, lililotoholewa moja kwa moja kutoka neno la Misri wḥ3t au Demotic wḥỉ.

Oasisi ya Huacachina katika Ica, Peru

Oasisi hutokana na mito iliyo chini ya ardhi au aquifer kama vile artesian aquifer, ambapo maji yanaweza kufikia juu kwa shinikizo la kimaumbile au kwa watu kuchimba visima. Gharika fupi za mara kwa mara hutoa maji chini ya ardhi na kuendeleza oasisi, kama vile Tuat. Miamba na mawe iliyo chini ya ardhi na isiyopenyeza maji inaweza kuyateka maji na kuyahifadhi katika mifuko; au katika sehemu ndefu chini ya ardhi zenye maeneo hafifu au mitaro ya volkeno maji yanaweza kukusanyika na kububujika juu ya ardhi. Matukio yoyote ya maji hutumiwa na ndege wakihama na pia kupitisha mbegu pamoja na mavi yao ambazo hukua kandokando ya maji hayo na kutengeneza Oasisi.

Kupanda mimea hariri

 
Oasisi katika sehemu ya Sahara ya Libya

Watu wanaoishi katika Oasisi hawana budi kusimamia kwa makini matumizi ya ardhi na maji; mashamba lazima yanyunyiziwe maji ili kukuza mimea kama vile mitende, mitini, mizeituni na miaprikoti. Mmea muhimu zaidi katika Oasisi ni mitende ambao hutengeneza safu ya juu. Mitende hiyo hutoa kivuli kwa miti midogo kama vile ya Peach, ambayo huwa katika safu ya katikati. Kwa kupanda mimea katika matabaka mbalimbali, wakulima hutumia ardhi na maji bora zaidi. Mboga nyingi pia hukuzwa na baadhi ya nafaka, kama vile ngano, shayiri na mtama hukuzwa katika maeneo yenye unyevu zaidi. [1]

Oasisi maarufu hariri

Afrika hariri

Amerika hariri

 
Fish Springs National Wildlife Refuge, Utah, Marekani.

Asia hariri

 
Ein Gedi, Israeli

Australasia hariri

Ulaya hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri