Papa Klementi II (10059 Oktoba 1047) alikuwa Papa kuanzia tarehe 24 Desemba 1046 hadi kifo chake[1]. Alitokea Saksonia, Ujerumani[2].

Papa Klementi II.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Suidger wa Morsleben und Hornburg. Alichaguliwa kwenye sinodi ya Sutri iliyoitishwa na mfalme Heinrich III wa Ujerumani wakati kulikuwa na watu watatu waliowahi kuchaguliwa kuwa Papa na maaskofu tofauti. Sinodi iliwaondoa wote watatu na kumchagua askofu Mjerumani Suidger ambaye alichukua jina la Kipapa Klementi II.

Alimfuata Papa Gregori VI akafuatwa na Papa Benedikto IX.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Klementi II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.